Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 SEPTEMBA 2022

19 SEPTEMBA 2022

Pakua

Hii leo kwenye Habari za UN, Flora Nducha anaanza na Kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu elimu, akisema elimu ndio kitu ambacho kinaweza kuleta amani na maendeleo ya kudumu duniani. Kisha ni taarifa ya mahojiano na mchechemu wa vijana wa UNICEF nchini Tanzania, Emmanuel Msoka akisema “maneno ni rahisi lakini vitendo ni aghali,” hivyo vitendo vyahitajika ili kusongesha maendeleo ya kweli. Anapendekeza kurejeshwa kwa Baraza la Vijana nchini Tanzania. Makala tunasalia makao makuu ya Umoja wa Mataifa kukuletea mahojiano na kijana Cherinet Harifo kutoka Tigray nchini Ethiopia akitaka viongozi watatue changamoto ya elimu kwa kuzingatia hali halisi ya kila eneo. Mashinani tutasikia ripoti inayobainisha kuwa hata simu yako ya mkononi inaweza kugeuka kuwa kifaa cha kufuatilia Maisha yako bila wewe kujua . Karibu!

Audio Credit
FLORA NDUCHA
Audio Duration
12'4"