Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP28

Mkutano wa 23 wa UN wa Mabadiliko ya Tabianchi: COP28
30 Novemba - 12 Desemba 2023: Dubai, Falme za Kiarabu

...

Viwango vya joto duniani vikiwa vimeongezeka na kuvunja rekodi, na matukio ya kupindukia ya hali ya hewa yakileta madhara kwa binadamu duniani kote, mwaka huu mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28, ni fursa ya kipekee ya kubadili mwelekeo na kuchochea hatua za kukabili janga la tabianchi.

COP28 ni pahala ambako dunia itatathmini utekelezaji wa Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya Tabianchi – mkataba wa aina yake uliopitishwa mwaka 2015 na kuweka mwelekeo wa kupunguza kwa kiasi kikubwa viwango vya utoaji wa hewa chafuzi ili kulinda uhai wa binadamu na mbinu za kujipatia kipato.

Wakuu wa Nchi, mawaziri na washauri na wasuluhishi, sambamba na wanaharakati wa tabianchi, mameya, wawakilishi wa mashirika ya kiraa na maafisa watendaji wakuu wa mashirika wanakutana kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Novemba huko Dubai, Falme za Kiarabu (UAE), ikiwa ni kusanyiko kubwa zaidi la mwaka kuhusu hatua kwa tabianchi.

Mkunga akimhudumia mwanamke mjamzito katika chumba cha kujifungulia katika hospitali moja nchini Sudan Kusini.
© UNICEF/Mark Naftalin

COP28: WHO yasema afya ipatiwe kipaumbele kwenye mijadala

Kuelekea mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP28 huko Dubai, Falme za kiarabu tarehe 30 mwezi huu wa Novemba, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, limesema washiriki wanapaswa waelewe kuwa suala la afya ndilo linapaswa kuchochea majadiliano wakati huu ambapo janga la tabianchi linazidi kushamiri duniani kote. 

Sauti
2'23"
Unsplash/Andreas Chu

Mataifa lazima yaende mbali zaidi kuliko ahadi za sasa kutokomeza uzalishaji wa Hewa Chafuzi - UNEP

Wakati joto la ulimwengu na uzalishaji wa hewa chafuzi vikivunja rekodi katika mwaka huu wa 2023, Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) ya Pengo la Uzalishaji hewa chafuzi iliyotolewa leo Novemba 20 mjini Nairobi Kenya imeeleza kwamba imegundua kuwa ahadi za sasa chini ya Mkataba wa Paris zinaweka ulimwengu kwenye mstari wa ongezeko la joto la nyuzi joto 2.5 hadi 2.9 za Selsiasi zaidi ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda katika karne hii. 

Sauti
2'12"
Vijana wanaharakati wa tabianchi huko Maldives wakipaza sauti zao wakihimiza hatua za kukuza mazingira zichukuliwe..
© UNICEF/Pun

Uzalishaji wa hewa chafuzi: Mataifa lazima yaende mbali zaidi kuliko ahadi za sasa - UNEP

Wakati joto la ulimwengu na uzalishaji wa hewa chafuzi vikivunja rekodi katika mwaka huu wa 2023, Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) ya Pengo la Uzalishaji hewa chafuzi iliyotolewa leo Novemba 20 mjini Nairobi Kenya imeeleza kwamba imegundua kuwa ahadi za sasa chini ya Mkataba wa Paris zinaweka ulimwengu kwenye mstari wa ongezeko la joto la nyuzi joto 2.5 hadi 2.9 za Selsiasi zaidi ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda katika karne hii.

Sauti
2'12"
UN News/George Musubao

Umoja wa Mataifa unasimama na Afrika kutatua janga la tabianchi – Joyce Msuya

Ijumaa wiki ijayo yaani tarehe 24 vitaanzaa vikao vya awali kuelekea COP 28 ambao ni Mkutano wa  mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika Dubai huko Falme za Kiarabu mwishoni mwa mwezi huu kuanzia tarehe 30.

Kuelekea mkutano huu, Naibu wa Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Joyce Msuya ameutumia mwezi huu kufanya ziara katika nchi nne za kusini na mashariki mwa Afrika ambako amesisitiza dhamira ya Umoja wa Mataifa ya kusimama na watu na Serikali za ukanda huo wakati janga la tabianchi linafanya mahitaji ya kibinadamu kuwa ya juu zaidi.

Sauti
1'33"
Msichana mdogo akitembea katika kijiji kilichofurika cha Ulang huko Sudan Kusini
© UNICEF/UN0548109/Jan Grarup

Kuelekea COP28 Guterres ataka pengo la matamanio ya tabianchi lizibwe

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza kwamba  Mkutano wa  mabadiliko ya tabianchi COP28 utakaofanyika Dubai baadaye mwezi huu "lazima uwe mahali pa kuziba kwa haraka pengo la matarajio ya hali ya hewa duniani wakati uzalishaji wa gesi chafuzi ukiendelea kuongezeka na changamoto za mabadiliko ya tabianchi zikiongezeka.

Msichana mdogo nchini Zimbabwe anakunywa maji safi na salama kutoka kwenye kisima kilichorekebishwa kwa msaada wa Umoja wa Mataifa.
© UNICEF/Karin Schermbrucker

Ripoti: Mtoto 1 kati ya 3 anakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji - UNICEF

Mtoto mmoja kati ya Watoto watatu au sawa na watoto milioni 739 duniani kote - tayari wanaishi katika maeneo yaliyo na uhaba mkubwa au wa juu sana wa maji, na mabadiliko ya tabianchi yanatishia kufanya hali hii kuwa mbaya zaidi, imebainisha ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Jumatatu kwa saa za New York, Marekani.

Sauti
1'49"