Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP28 inahusu hatua si siasa wala kupata alama: Mkuu wa UN wa tabianchi

Simon Stiell, Katibu Mtendaji wa UNFCCC akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28, kwenye Expo City huko Dubai, Falme za Kiarabu.
COP28/Christophe Viseux
Simon Stiell, Katibu Mtendaji wa UNFCCC akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28, kwenye Expo City huko Dubai, Falme za Kiarabu.

COP28 inahusu hatua si siasa wala kupata alama: Mkuu wa UN wa tabianchi

Tabianchi na mazingira

Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi Simon Stiell leo amewaambia wajumbe wanaoshiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 kuwa hawako Dubai kupata alama na kucheza siasa za chini kabisa lazima wachukue hatua kabambe katika kuzuia ongezeko la joto duniani na kumaliza janga la mabadiliko ya tabianchi”.

Ujumbe mzito wa Bwana Stiell kwa wazungumzaji wa serikali unakuja wakati mkutano huo wa karibuni zaidi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi unaoendelea katika mji mkuu wa Falme za nchi za Kiarabu (UAE) huko, Dubai, tangu Alhamisi iliyopita, ukifikia nusu ya makubaliano ya ufadhili wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na hatima ya nishati ya mafuta kisukuku bado ikiwa njiapanda.

Bwana Stiel ambaye ni Katibu Mtendaji wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, ambao unawezesha COP28 amesisitiza kuwa "Serikali zote lazima ziwape wajadili wao maagizo bayana. Tunahitaji matamanio ya juu zaidi, sio kujipatia alama au siasa za chini kabisa.”

Nia njema haitapunguza uzalishaji wa hewa chafuzi kwa nusu

Akirejelea ushindi wa awali kwa ajili ya hasara na uharibifu siku ya ufunguzi wa mkutano huo, amekiri kwamba mpango uliosubiriwa kwa muda mrefu umeipa COP28 chemchemi katika hatua yake.

Lakini "ni mwanzo tu," ameonya, na kuongeza kuwa "Tutakuwa tunajidanganya ikiwa tunafikiri ni tiki kwenye kisanduku cha fedha na usaidizi katika COP hii. Hatua zaidi zinahitajika."

Amewataka wajumbe kuangalia kwa kina kazi halisi iliyo mbele yao, kwa sababu "nia njema haitapunguza kwa nusu uzalishaji wa hewa chafuzi katika muongo huu au kuokoa maisha kwa sasa. Tunahitaji kuimarisha hali ya uwazi, na kutoa ahadi yetu ya kufadhili hatua za tabianchi duniani kote".

Hatua kubwa zinahitajika katika masuala ya fedha

Akitoa maono yake kwa ajili ya duru inayofuata ya mazungumzo ya mabadiliko ya tabianchi, bwana Stiel amesema "Hatua kubwa za kifedha zinaweza kuleta matokeo ya mstari wa mbele, ambayo ni kuwezesha kwa kiasi kikubwa hatua za mabadiliko ya tabianchi. Majadiliano lazima yaweke mbele na kuwa kitovu”

Uhakiki wa kimataifa

Kulingana na Bwana Stiell, uhakiki wa kimatifa au Global Stocktake ndio chombo cha kuleta mabadiliko ya tabianchi kwenye mstari unatakiwa.

Kwa maneno rahisi, mchakato wa kuhesabu hatua zilizopigwa utapitia ni kiasi gani cha maendeleo ambacho nchi zimefanya na kubainisha palipo na mapungufu katika kufikia malengo yaliyowekwa na makubaliano ya kihistoria ya Paris ya Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2015, na matokeo yake yataweka ramani ya hatua ya kuharakishwa kwa hatua dhidi ya tabianchi kwa miaka ijayo.

"Kwenye uhakiki wa kimataifa, tuna maandishi ya kuanzia kwenye jedwali  Lakini ni begi la orodha za matamanio na ambayo ni mazito kuyatekeleza. Jambo kuu sasa ni kupembua ngano kutoka kwa makapi. Ikiwa tunataka kuokoa maisha sasa na kufikia lengo la nyuzi joto 1.5 matokeo ya juu zaidi ya COP lazima yabaki kuwa kipaumbele na kitovu."

Kasi isiyo ya kawaida kwa hatua za mabadiliko ya tabianchi

Bwana Stiell amesisitiza kuwa kufikia mwisho wa wiki ijayo, wakati mkutano huo unakaribia kufungwa, COP28 lazima itoe hatua za kasi ya treni ya risasi ili kuharakisha hatua za mabadiliko ya tabianchi.

"Kwa sasa tuna msururu wa zamani wa nyimbo mbovu." Amesema Steil na kuongeza kuwa teknolojia na suluhu zipo, na zana zote ziko kwenye meza.

"Ni wakati wa serikali na wadau wote kuzichukua na kuzifanyia kazi."