Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Historia yaandikwa COP28 kwa kupitishwa kwa makubaliano ya fidia kwa hasara na uharibifu.

Muonekano wa Jumba la Al Wasl Dome katika Jiji la Maonesho huko Dubai, Falme za Kiarabu, ambalo ni mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchia COP28.
COP28/Neville Hopwood
Muonekano wa Jumba la Al Wasl Dome katika Jiji la Maonesho huko Dubai, Falme za Kiarabu, ambalo ni mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchia COP28.

Historia yaandikwa COP28 kwa kupitishwa kwa makubaliano ya fidia kwa hasara na uharibifu.

Tabianchi na mazingira

Wajumbe wanaokutana Dubai wamekubali hii leo Alhamisi kuanza kufanya kazi kwa mfuko utakaosaidia kulipa fidia nchi zinazopata hasara na uharibifu kutokana na mabadiliko ya tabianchi, hatua ya kihistoria, katika siku ya kwanz aya mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya TAbianchi, UNFCCC. 

“Habari za leo kuhusu hasara na uharibifu utokanao na mabadiliko ya tabianchi, zinapatia mkutano huu wa UN wa tabianchi mwanzo mzuri. Serikali zote na waongoza majadiliano lazima watumie fursa hii kuleta matokeo makubwa hapa Dubai,” amesema Katibu Mtendaji wa UNFCCC Simon Stiell wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo ndipo tangazo la kupitishwa kwa makubaliano lilifanyika. 

Wakimbizi wa Sudan wakiwasili katika eneo lililofurika la Adre nchini Chad
© UNHCR/Jutta Seidel
Wakimbizi wa Sudan wakiwasili katika eneo lililofurika la Adre nchini Chad

Guterres asema sasa serikali zichangie mfuko huo 

Kupitia mtandao wa X (Zamani Twitter) Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  António Guterres naye pia  amekaribisha makubaliano hayo  ya kuanza kutekelezwa kwa mfuko huo akisema ni mbinu muhimu ya kuleta haki kwa tabianchi. Amesihi viongozi kusaidia mfuko huo na kupatia COP28 mwanzo thabiti. 

Mfuko huo umekuwa ni ombi la muda mrefu la nchi zinazoendleea ambazo ndizo zinakabiliana zaidi na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, zikigharimika kwa kiasi kikubwa na matukio ya kupindukia ya hali ya hewa kama vile joto kali, ukame na mafuriko. 

Kufuatia mijadala mikali na ya muda mrefu kwenye vikao vya aina hii vya kila mwaka, nchi tajiri ziliongeza usaidizi wao kwa mfuko huo wakati wa mkutano waCOP27 huko Sharm el-Sheikh nchini Misri. 

UAE, Ujerumani, Japani na Marekani zatangaza michango yao 

Imeripotiwa kuwa, Sultan al-Jaber, ambaye ndiye Rais wa COP28  amesema nchi yake, yaani Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) itachangia dola milioni 100 kwenye mfuko huo. 

Ujerumani nayo imeripotiwa kutangaza ahadi ya dola milioni 100 kwa mfuko huo, huku Marekani na Japan nazo pia zikitangaza michango yao. 

Simon Stiell, Katibu Mtendaji wa UNFCCC, ambao ni Mkataba wa Kimataifa wa mabadilik ya tabianchi akihutubia katika ufunguizi rasmi wa mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa UNFCCC huko Dubai, Falme za kiarabu.
COP28/Christopher Pike
Simon Stiell, Katibu Mtendaji wa UNFCCC, ambao ni Mkataba wa Kimataifa wa mabadilik ya tabianchi akihutubia katika ufunguizi rasmi wa mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa UNFCCC huko Dubai, Falme za kiarabu.

Mapema akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mkutano huo wa COP28, Katibu Mtendaji wa UNFCCC Simon Stiell alionya kwamba dunia inachukua hatua pole pole sawa na  “hatua za mtoto” wakati huu inakabiliwa na janga la kutisha dhidi ya sayari, janga linalotaka hatua za kijasiri kwa sasa. 

Tunatembea hatua za mtoto mdogo na tunachukua muda mrefu kufika mbali,” kupata majawabu bora kwenye madhara makubwa ya tabianchi yanayotukabili,” amesema Bwana Stiell.

Mkutano huu unaotarajiwa kuendelea hadi tarehe 12 mwezi Desemba, unafanyika kwenye kampasi ya jiji la maonesho, Expo City lililopambwa na miti na mimea. Eneo hili liko kwenye viunga vya mji wa Dubai, na linatarajiwa kuwa mgeni wa zaidi ya washiriki 70,000.

Na musa mchache uliopita kabla ya ufunguzi wa mkutano huo, shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa, WMO limetoa ripoti yake ya awali ikisema kuwa kipindi hiki kimegubikwa na viwango vya  hali ya hewa vya kupitiliza vikivunja rekodi na kuacha hali ya kukata tamaa.

Ulimwenguni, halijoto inafikia viwango vya juu kuwahi kurekodiwa.
© Unsplash/Raphael Wild
Ulimwenguni, halijoto inafikia viwango vya juu kuwahi kurekodiwa.

Nini kiko hatarini

Katika hotuba yake hii leo, Bwana Stiell ameeleza kile kilichoko hatarini. “Huu umekuwa ni mwaka wenye kiwango cha juu cha joto zaidi kwa binadamu. Rekodi nyingi za viwango vya juu vya joto zimevunjwa,” amesema Bwana Stiell, akiongeza: tunacheza na uhai wa watu na mbinu zao za kujipatia kipato.”

“Sayansi inatueleza kuwa tuna miaka takribani sita kabla ya kufikia uwezo wa mwisho kabisa wa sayari yetu kuhimili uchafuzi wetu. Kabla ya kuvuka kiwango cha nyuzi joto 1.5 katika kipimo cha Selsiyasi,” ameonya, akigusia moja ya malengo makubwa ya mkataba wa Mkataba wa Paris. 

Ripoti kuelekea COP28 zinaonesha hali ni tete

Kinachotisha zaidi, ni msururu wa ripoti zilizochapishwa kuelekea COP28 ambazo zimeonesha kuwa dunia iko mbali zaidi katika kufanikisha malengo ya tabianchi, na bila malengo mazito na ya kina, dunia inaelekea kwenye kiwango cha joto kuongezeka kwa nyuzi joto 3 katika kipimo cha Selsiyasi ifikapo mwishoni mwa karne hii ya 21.

Katika mazingira hara, Bwana Stiell ametoa wito kwa nchi kuwasilisha Ahadi za Michango ya Kitaifa, NDCs, au mikakati ya kitaifa kuhusu tabianchi, ambapo kila lengo ifikapo mwaka 2025 – kuhusu fedha, kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabianchi lazima yalenge kutovukisha kiwago cha joto juu ya nyuzi joto 1.5 katika kipimo cha Selsiyasi.