Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP28

Mkutano wa 23 wa UN wa Mabadiliko ya Tabianchi: COP28
30 Novemba - 12 Desemba 2023: Dubai, Falme za Kiarabu

...

Viwango vya joto duniani vikiwa vimeongezeka na kuvunja rekodi, na matukio ya kupindukia ya hali ya hewa yakileta madhara kwa binadamu duniani kote, mwaka huu mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28, ni fursa ya kipekee ya kubadili mwelekeo na kuchochea hatua za kukabili janga la tabianchi.

COP28 ni pahala ambako dunia itatathmini utekelezaji wa Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya Tabianchi – mkataba wa aina yake uliopitishwa mwaka 2015 na kuweka mwelekeo wa kupunguza kwa kiasi kikubwa viwango vya utoaji wa hewa chafuzi ili kulinda uhai wa binadamu na mbinu za kujipatia kipato.

Wakuu wa Nchi, mawaziri na washauri na wasuluhishi, sambamba na wanaharakati wa tabianchi, mameya, wawakilishi wa mashirika ya kiraa na maafisa watendaji wakuu wa mashirika wanakutana kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Novemba huko Dubai, Falme za Kiarabu (UAE), ikiwa ni kusanyiko kubwa zaidi la mwaka kuhusu hatua kwa tabianchi.

Marynsia Mangu

Heko Marynsia kwa ushindi wa tuzo COP28

Marynsia Mangu, mmoja wa washiriki wa COP28 au mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC uliofanyika huko Dubai, Falme za Kiarabu, ambaye ameondoka akiwa amebeba tuzo. Tuzo inayodhihirisha utendaji wake yeye kama Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Success Hands Tanzania.  Shirika hili linahusika na kuwajengea watoto tabia ya kupenda kusoma vitabu, tena tangu wakiwa tumboni mwa mama zao. Idhaa ya Umoja wa Mataifa ilitaka kufahamu mengi kutoka kwake ikiwemo ni tuzo gani ameshinda.

Audio Duration
3'58"
UNFCCC/Kiara Worth

UN: COP28 yafunga pazia kwa muafaka wa kuanza kutokomeza mafuta kisuskuku

Hatimaye mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28, leo umekunja jamvi mjini Dubai huko Umoja w Falme za Kiarabu (UAE) kwa muafaka ambao Umoja wa Mataifa unasema unatoa ishara ya kuanza kutokomezwa kwa mafuta kisukuku au Fossil Fuels, ingawa baadhi ya nchi za visiwa vidogo vinavyoendelea ikiwemo Samoa zinaona muafaka huo hautoshelezi kuwalinda kikamilifu dhidi ya tabianchi.

Sauti
2'47"
Rais wa COP28, Sultan Al Jaber (katikati), Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa, Simon Stiell (wa nne kutoka kushoto) na washiriki wengine wakiwa jukwaani wakati wa Kufunga Mkataba wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28,…
COP28/Christopher Pike

COP28 yakunja jamvi kwa muafaka wa mataifa  kuanza kuondokana na mafuta kisukuku

Mataifa hii leo katika mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 uliokunja jamvi mjini Dubai Falme za nchi za Kiarabu wamepitisha makubaliano yanayotoa mwelekeo wa mpito wa kuondokana na mafuta kisukuku au fossil fuel  yakiwa ni ya kwanza kwa mkutano huo wa Umoja wa Mataifa lakini muafaka huo haukutimiza wito uliotakwa na wengi kwa muda mrefu wa "kukomesha matumizi ya mafuta kisukuku, makaa ya mawe na gesi.”

Sauti
2'47"