INC-3: Chombo cha kimataifa cha kisheria kudhibiti uchafuzi unaotokana na plastiki kuundwa

INC-3: Chombo cha kimataifa cha kisheria kudhibiti uchafuzi unaotokana na plastiki kuundwa
Kikao cha tatu cha Kamati ya Majadiliano ya Kiserikali kuunda chombo cha kisheria cha kimataifa kuhusu uchafuzi wa mazingira unaotokana na plastiki, ikiwa ni pamoja na mazingira ya baharini (INC-3), kimefunguliwa leo (13 Nov) katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Wanachama wa INC-3 wataanza mazungumzo kwa misingi ya Nakala ya Rasimu iliyotayarishwa na Mwenyekiti wa INC. INC-3 ni inaashiria safari kuelekea mkataba wa kimataifa. Inafuatia duru mbili za awali za mazungumzo: INC-1, ambayo yalifanyika Punta del Este, Uruguay, mnamo Novemba 2022, na INC-2, ambayo ilifanyika Paris mnamo Juni.
Rais Ruto
Katika ufunguzi leo wa mkutano huo utakaofanyika hadi tarehe 19 Novemba hii, William Ruto, Rais wa Jamhuri ya Kenya amesema, "Ili kukabiliana na uchafuzi wa mazingira unaotokana na plastiki, ubinadamu lazima ubadilike. Lazima tubadilishe jinsi tunavyotumia, jinsi tunavyozalisha, na jinsi tunavyotupa taka zetu. Huu ndio ukweli wa ulimwengu wetu. Mabadiliko hayaepukiki. Mkataba huu, chombo hiki ambacho tunafanyia kazi, ni kipande cha kwanza katika mabadiliko haya."
Mkuu wa UNEP
Kwa upande wake Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira (UNEP amesema, "Azimio ambalo mlipitisha katika UNEA 5.2 lilitaka chombo ambacho ni na ninanukuu, kwa kuzingatia hatua Madhubuti ya inayoshughulikia mzunguko kamili wa maisha ya plastiki, mwisho wa kunukuu. Si chombo kinachoshughulikia uchafuzi wa plastiki kutokana na kuchakata tena au usimamizi wa taka pekee. Mzunguko kamili wa maisha. Na hii inamaanisha kufikiria upya kila kitu kwenye mnyororo kutoka kwa ‘polima’ hadi uzalishaji, kutoka kwa bidhaa hadi ufungashaji. Tunahitaji kutumia vifaa vichache, plastiki kidogo na bila kemikali hatari. Tunahitaji kuhakikisha kuwa tunatumia na kutumia tena na kuchakata rasilimali kwa ufanisi zaidi na kutupa kile kilichosalia kwa usalama.”
Gustavo Adolfo Meza-Cuadra Velasquez
Mwenyekiti, Kamati ya Majadiliano ya Kiserikali (ING), Gustavo Adolfo Meza-Cuadra Velasquez yeye anasema ni matumaini yake kuwa, “hadi mwisho wa kikao kamati itakubaliana kuhusu agizo la rasimu iliyorekebishwa na uwezekano wa kufanya kazi za pamoja ili kujiandaa na kikao cha nne na cha tano. Nina imani kwamba tunaweza kufanya maendeleo makubwa hapa katika kikao chetu cha tatu na kufaidika na ari ya maafikiano ya Nairobi ambayo ilituletea mamlaka ya kujadili chombo hiki.”
Vikao vingine viwili vya INC vimepangwa kufanyika mwaka wa 2024. Azimio namba 5/14 la Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa lilimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP kuitisha kamati ya majadiliano baina ya serikali, ili kuanza kazi yake katika nusu ya pili ya 2022, kwa nia ya kukamilisha kazi yake kufikia mwisho wa mwaka 2024.
INC ina jukumu la kuunda chombo cha kisheria cha kimataifa kuhusu uchafuzi unaotokana na plastiki, ikiwa ni pamoja na mazingira ya baharini, ambayo tangu sasa inajulikana kama "chombo", ambayo inaweza kujumuisha mbinu za kishria na za hiari, kwa kuzingatia mbinu ya kina ambayo inashughulikia mzunguko kamili wa maisha. ya plastiki.