Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola trilioni 7 hutumika kila mwaka katika uwekezaji unaoathiri mazingira: UN Ripoti

Bustani ya nyasi bahari - upanuzi wa kijani kibichi, chipukizi na maua kama nyasi - ni suluhisho bora kwa mabadiliko ya hali ya hewa kwa msingi wa asili.
© Unsplash/Benjamin L. Jones
Bustani ya nyasi bahari - upanuzi wa kijani kibichi, chipukizi na maua kama nyasi - ni suluhisho bora kwa mabadiliko ya hali ya hewa kwa msingi wa asili.

Dola trilioni 7 hutumika kila mwaka katika uwekezaji unaoathiri mazingira: UN Ripoti

Tabianchi na mazingira

Takriban dola trilioni 7 za fedha za umma na za sekta binafsi kila mwaka zinasaidia shughuli zenye athari mbaya kwa mazingira zinazochochea moja kwa moja mabadiliko ya tabianchi  takriban mara 30 ya kiasi kinachotumiwa katika ufumbuzi suluhu za mazingira kila mwaka, imesema ripoti ya kushangaza ya Umoja wa Mataifa iliyozinduliwa leo Jumamosi kwenye mkutano wa Umoja Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi  COP28 huko Dubai.

Ripoti hiyo ya shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, pia imefichua kuwa licha ya miongo kadhaa ya wito wa kupunguza mtiririko wa fedha kuelekea sekta zinazodhuru baadhi ya maliasili muhimu za binadamu, uwekezaji huo kwa sasa unachangia asilimia 7 ya Pato la Taifa.

Ripoti hiyo “Hali ya Fedha kwa ajili ya Mazingira kwa mwaka huu” ndiyo ripoti ya kwanza kama hiyo kuangazia kile kinachojulikana kama "mitiririko ya kifedha yenye madhara kwa maliasili" na inasisitiza udharura wa kushughulikia migogoro iliyounganishwa ya mabadiliko ya tabianchi, upotevu wa bayoanuwai, na uharibifu wa ardhi.

Ripoti hiyo, iliyozinduliwa sanjari na siku iliyotengwa katika mkutano waCOP28 kwa ajili ya majadiliano juu ya asili na matumizi ya ardhi, pia imeonyesha ukweli kwamba uwekezaji huu ulipunguza kiasi cha mwaka kinachowekezwa katika ufumbuzi Edgard suluhu za asili, ambao ulifikia takriban dola bilioni 200 mwaka uliopita.

Dola bilioni 5 za mtiririko huu wa kifedha usio na maslahi kwa asili hutoka kwa sekta binafsi, ambayo ni kubwa mara 140 kuliko uwekezaji binafsi katika suluhu za asili, na karibu nusu ya hiyo inatokana na tasnia 5 pekee ambazo ni ujenzi, huduma za nishati ya umeme, mali isiyohamishika, mafuta na gesi, chakula na tumbaku.

Dola trilioni 1.7 zinazosalia hutumiwa na serikali kwa ruzuku zinazodhuru mazingira, ambazo ni mara 10 ya kiasi wanachotumia katika uwekezaji kwa mazingira.

Kituo cha Sola kwenye mkutano wa dubai COP28
Credit: Noor Nation
Kituo cha Sola kwenye mkutano wa dubai COP28

Ufadhili unaojali mazingira

Mmoja wa washirika wa UNEP waliochangia katika ripoti hiyo ni Global Canopy, shirika lisilo la kiserikali linaloendeshwa na takwimu ambalo linalenga vichochezi vya soko vinavyoathiri vibaya maliasili. 

Mkurugenzi Mtendaji Edgard shirika hilo Niki Mardas, ameiambia UN News kwamba kuna kundi la makampuni au taasisi za fedha ambazo zinaweza kuwa zinawekeza katika mazingira chanya na kupiga kelele kubwa kuhusu hilo, lakini hata hawatambui walivyokatika hatari ya uwekezaji wa athari hasi chini ya minyororo yao ya usambazaji."

Amesisitiza kuwa, pamoja na kwamba kampuni hizo zinapaswa kuendelea kufanya uwekezaji chanya, pia zinapaswa kufanya kazi ngumu na kubwa ya kuelewa ni jinsi gani wanaendesha tatizo hilo.

Lazima waanze kushughulikia hilo "sio kwa kutoka nje na sio kwa kutorosha, lakini kwa kushirikisha kampuni katika porfolio zao, kwa kushirikisha makampuni katika minyororo yao ya ugavi ili wabadilishe shughuli zao na tabia zao".

Bwana Mardas ametoa mfano wa kukabiliana na ukataji miti, ambao ndio "kiini" cha juhudi zozote za kufikia leo la kutochangia kabisa uzalishaji wa hewa ukaa lakini ni asilimia 20 tu ya taasisi zaidi ya 700 za kifedha ambazo zilitoa ahadi za hali ya juu za kutozalisha kabisa hewa ukaa kama sehemu ya makubaliano ya Glasgow ya Muungano wa kifedha "wamechukua hatua yoyote juu ya ukataji miti. 

Amesema"Hatua moja kubwa tunayoweza kuchukua kwa asili, mabadiliko ya tabianchi na watu ni ufadhili unaojali mazingira. Tunahitaji kufadhili mazingira lakini pia tunahitaji kuwekakiasi hicho cha dola trilioni 7 katika mazingira. Vinginevyo, tutakwama katika kitanzi hiki kila wakati,” ameongeza.

Kilimo asilia cha kisasa cha mbogamboga Pakistan
Muhammad Faisal
Kilimo asilia cha kisasa cha mbogamboga Pakistan

Kubadili mwelekeo

Katika mkutano na waandishi wa habari huko Dubai, mkuu wa kitengo cha hali ya hewa cha UNEP, Mirey Atallah, amesema ripoti hiyo inaonyesha kuwa janga la mabadiliko ya tabianchi badolinazidi juhudi za kulidhibiti.

Amesema fedha ni "kiwezeshaji kikubwa, na bila fedha za kuingia katika mwelekeo sahihi, hatuwezi kufikia malengo tuliyoweka" katika mkutano wa dunia wa 1992 huko Rio ili kushughulikia changamoto zilizounganishwa za mabadiliko ya tabianchi, kuenea kwa jangwa na uharibifu wa viumbe hai.

Ingawa ripoti hiyo inaweza kutoa hitimisho la kutisha sana, Bibi Atallah amesema UNEP inataka kutumia takwimu kuonyesha kwamba pesa zinazotumiwa kudhuru asili zinaweza na lazima zielekezwe ili kuwa na matokeo chanya na akasisitiza kuwa COP28 lazima iwe hatua ya mabadiliko.

Akizungumza na UN News, afisa huyo wa UNEP amesema ufadhili duni wa suluhu za asili hautokani na ukosefu wa fedha, bali ni kwamba pesa zinaenda katika mwelekeo mbaya".

Amesema kushawishi kampuni binafsi kufanya uwekezaji sahihi kunahitaji kuweka mifumo muhimu ya kisheria kusaidia kuelekeza fedha kwenye suluhu za asili.

Bibi Atallah amebainisha kuwa baadhi ya taasisi za fedha za binafsi tayari zimeanza kuzingatia athari za mabadiliko ya tabianchi zinapofikiwa kwa ajili ya mikopo, ambayo inaweza kusaidia "kugeuza wimbi la uwekezaji".