Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mifumo bora ya chakula kusaidia vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi : FAO

Mifumo bora ya kilimo ni muhimu katika kuongeza mazao kwa wakulima na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
© FAO
Mifumo bora ya kilimo ni muhimu katika kuongeza mazao kwa wakulima na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Mifumo bora ya chakula kusaidia vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi : FAO

Tabianchi na mazingira

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO, QU Dongyu, akizungumza leo jijini Roma, nchini Italia, amesema “Wakati dunia inakabiliana na uharaka wa hatua dhidi ya tabianchi, FAO itaangazia katika mkutano ujao wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 kuhusu uwezo wa kipekee wa mifumo ya chakula cha kilimo kama msingi wa suluhu endelevu.” 

QU ataongoza ujumbe wa FAO katika mkutano huo wa kimataifa utakayofanyika mwaka huu Dubai, katika Falme za nchi za Kiarabu, kuanzia Novemba 30 hadi Desemba 12, na ukitarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu 65,000, zikiwemo nchi wanachama. 

Wanachama wa Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC, karibu viongozi 150 wa dunia, sekta binafsi, vijana, wanasayansi wa mabadiliko ya tabaianchi, watu wa jamii za asili, waandishi wa habari na watetezi mbalimbali wenye ushawishi wa tabianchi kama vile Papa Francis na Mfalme Charles wa Uingereza.

Uzalishaji na utumiaji wa chakula ni chachu ya afya na mazingira
© Unsplash/Anna Pelzer
Uzalishaji na utumiaji wa chakula ni chachu ya afya na mazingira

Tabianchi na chakula ni lila na fila havitengamani

Bwana. QU ameendelea kusema kuwa “majanga ya mabadiliko yatabianchi na chakula havitenganishwi. Uwekezaji katika mifumo ya kilimo na maeneo ya vijijini hutengeneza suluhu madhubuti ya kushughulikia athari za mjanga la mabadiliko ya tabianchi.”

Katika COP28 FAO itaangazia kwa utaratibu jinsi mabadiliko ya mifumo ya kilimo unavyoharakisha hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kwa manufaa ya watu na ustawi na sayari. 

Majadiliano na mazungumzo mwaka huu yamewekwa ili kujumuisha mienendo muhimu ya kazi, inayolenga kuleta maendeleo makubwa katika masuala muhimu. 

Moja ni kukamilisha kituo cha fedha cha hasara na uharibifu kilichokubaliwa kuanzishwa katika COP27 ili kusaidia jamii zilizo katika mazingira magumu katika mstari wa mbele wa athari, ikiwa ni pamoja na wakulima, katika kukabiliana na athari za haraka za mabadiliko ya tabianchi. 

Lengo lingine muhimu ni kusonga mbele kuelekea lengo la kifedha la kimataifa kusaidia nchi zinazoendelea katika juhudi zao za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. 

Na pia kuharakisha hatua za kuhamia kwenye nishati safi na hatua ambazo ni za haki, na pia kushughulikia pengo la uzalishaji, pia ni maeneo muhimu ambayo yatazingatiwa, miongoni mwa mengine.

Kilimo cha kisasa cha mboga kutoka kikundi cha ushirika cha Agro Pour Tout (APT) Benin
© UN Benin/DR
Kilimo cha kisasa cha mboga kutoka kikundi cha ushirika cha Agro Pour Tout (APT) Benin

Msaada kwa wanachama

QU ameendelea kusema kuwa COP28 pia itashuhudia hitimisho la uorodheshaji wa kwanza kabisa wa hatua zilizochukuliwa duniani, mchakato unaofanywa na nchi na wadau kutathmini ni wapi maendeleo yanadumaa, au la, kufikia malengo ya Mkataba wa Paris. Mchakato huo utamalizika kwa uamuzi ambao unatarajiwa kuongezwa ili kuharakisha azma katika awamu inayofuata ya mipango ya utekelezaji wa mabadiliko ya tabianchi itakayotolewa mwaka wa 2025, kitu ambacho FAO imekuwa ikisaidia nchi. 

FAO itawasaidia wanachama wake wakati wa michakato hii, ikiwa ni pamoja na majadiliano juu ya kazi ya pamoja ya Sharm el-Sheikh kuhusu utekelezaji wa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, juu ya kilimo na uhakika wa chakula ambayo huleta mjadala wa ufumbuzi wa mifumo ya kilimo ndani ya kitovu cha mazungumzo.

Hali kadhalika, QU imehitimisha kwa kusema kuwa FAO pia imejitolea kusaidia nchi katika utekelezaji wa ufumbuzi wa mifumo ya kilimo cha mazao kulingana na Azimio la Falme za nchi za Kiarabu litakalotolewa kuhusu kilimo endelevu, mifumo ya chakula yenye mnepo, na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. 

Azimio hilo litazinduliwa huko Dubai kama sehemu ya ajenda kabambe ya ofisi ya Rais kuhusu chakula na kilimo ambayo itakuwa kipengele kikuu cha mkutano wa kilele wa utekelezaji wa tabianchi duniani tarehe 1 Desemba na Siku ya Chakula, Kilimo na Maji tarehe 10 Desemba.