Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP28

Mkutano wa 23 wa UN wa Mabadiliko ya Tabianchi: COP28
30 Novemba - 12 Desemba 2023: Dubai, Falme za Kiarabu

...

Viwango vya joto duniani vikiwa vimeongezeka na kuvunja rekodi, na matukio ya kupindukia ya hali ya hewa yakileta madhara kwa binadamu duniani kote, mwaka huu mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28, ni fursa ya kipekee ya kubadili mwelekeo na kuchochea hatua za kukabili janga la tabianchi.

COP28 ni pahala ambako dunia itatathmini utekelezaji wa Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya Tabianchi – mkataba wa aina yake uliopitishwa mwaka 2015 na kuweka mwelekeo wa kupunguza kwa kiasi kikubwa viwango vya utoaji wa hewa chafuzi ili kulinda uhai wa binadamu na mbinu za kujipatia kipato.

Wakuu wa Nchi, mawaziri na washauri na wasuluhishi, sambamba na wanaharakati wa tabianchi, mameya, wawakilishi wa mashirika ya kiraa na maafisa watendaji wakuu wa mashirika wanakutana kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Novemba huko Dubai, Falme za Kiarabu (UAE), ikiwa ni kusanyiko kubwa zaidi la mwaka kuhusu hatua kwa tabianchi.

Msichana mdogo nchini Zimbabwe anakunywa maji safi na salama kutoka kwenye kisima kilichorekebishwa kwa msaada wa Umoja wa Mataifa.
© UNICEF/Karin Schermbrucker

Ripoti: Mtoto 1 kati ya 3 anakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji - UNICEF

Mtoto mmoja kati ya Watoto watatu au sawa na watoto milioni 739 duniani kote - tayari wanaishi katika maeneo yaliyo na uhaba mkubwa au wa juu sana wa maji, na mabadiliko ya tabianchi yanatishia kufanya hali hii kuwa mbaya zaidi, imebainisha ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Jumatatu kwa saa za New York, Marekani.

Sauti
1'49"