Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa unasimama na Afrika kutatua janga la tabianchi – Joyce Msuya

Umoja wa Mataifa unasimama na Afrika kutatua janga la tabianchi – Joyce Msuya

Pakua

Ijumaa wiki ijayo yaani tarehe 24 vitaanzaa vikao vya awali kuelekea COP 28 ambao ni Mkutano wa  mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika Dubai huko Falme za Kiarabu mwishoni mwa mwezi huu kuanzia tarehe 30.

Kuelekea mkutano huu, Naibu wa Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Joyce Msuya ameutumia mwezi huu kufanya ziara katika nchi nne za kusini na mashariki mwa Afrika ambako amesisitiza dhamira ya Umoja wa Mataifa ya kusimama na watu na Serikali za ukanda huo wakati janga la tabianchi linafanya mahitaji ya kibinadamu kuwa ya juu zaidi.

"Na nitamalizia kwa kusema jumuiya ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na NGOs, NGOs za kitaifa na kimataifa, tumejitolea kikamilifu kuendelea kuunga mkono na kukamilisha juhudi za mamlaka zinazojaribu kuokoa maisha, na pia tutaendelea kufanya kazi na wadau wetu wa maendeleo katika mnepo.”

Alipokuwa nchini Msumbiji, nchi ya kwanza katika ziara yake kabla ya Kwenda Tanzania, Kenya na Botswana, Bi Msuya alijionea jinsi athari ya pamoja ya vimbunga, migogoro na mabadiliko ya tabianchi yameweka zaidi ya watu milioni 2 katika mahitaji makubwa ya  kibinadamu.

"Nimejawa na matumaini kwa sababu ya ujasiri wa watu niliokutana nao, watoto ambao nimecheza nao, wataalamu wa tiba ambao nimezungumza nao na maafisa wa kibinadamu wa wilaya ambao wanajitoa sana."

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
1'33"
Photo Credit
UN News/George Musubao