Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa uzalishaji bora wa chakula kunusuru lengo la kuhakikisha nyuzijoto 1.5: COP28

Mtazamo katika mkutano wa wakulima na wazalishaji wa asili katika mkutano wa COP28 mjini Dubai falme za nchi za Kiarabu
COP28/Christophe Viseux
Mtazamo katika mkutano wa wakulima na wazalishaji wa asili katika mkutano wa COP28 mjini Dubai falme za nchi za Kiarabu

Mpango wa uzalishaji bora wa chakula kunusuru lengo la kuhakikisha nyuzijoto 1.5: COP28

Tabianchi na mazingira

Wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 ukielekea katika siku zake za mwisho huko Dubai, mrengo wa kilimo wa Umoja wa Mataifa umezindua leo Jumapili ukiwa ni mpango wa msingi ambao unatazamia kubadilisha mifumo ya kilimo ya chakula kutoka kuwa mtoaji mkubwa wa hewa ukaa hadi shimo la kufonza hewa hiyo ukaa ifikapo 2050.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO “limeainisha maeneo 10 ya kipaumbele kama vile mifugo, udongo na maji, mazao, lishe na uvuvi ambapo kufuata ramani ya mwelekeo iliyowekwa kunaweza kusaidia kusukuma ulimwengu karibu na kufikia lengo la kutokomeza kabisa njaa, ambalo ni lengo la pili kati ya Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs)”

Lengo: Ni kubadilisha mifumo ya chakula cha kilimo ambayo inajumuisha jinsi chakula tunachokula kinavyolimwa au kukuzwa, jinsi kinavyosafirishwa, na jinsi gani na mahali tunapotupa kuongezeka kwa uvunaji kutoka wa hewa ukaa kutoka kuwa mzalishaji wa hewa hiyo hadi mvunaji ifikapo 2050, na kukamata gigatani 1.5 ya uzalishaji wa gesi chafuzi kila mwaka.

Lengo: Kusaidia kuondoa njaa duniani bila kuifikisha sayari kwenye kikomo cha nyuzijoto 1.5 cha ongezeko la joto duniani kama ilivyowekwa na Mkataba wa Paris.

Katika mkutano huo wa COP28 wa Umoja wa Mataifa huko Dubai UN News imezungumza na David Laborde, Mkurugenzi wa Kitengo cha Uchumi wa Kilimo katika shirika la FAO, ambaye amesema ramani ya barabara hiyo imeundwa ili kuepusha "maangamizi na inatoa mwelekeo wa hatua za kuchukua leo katika njia ambayo inaweza kuwanufaisha wote sasa na katika siku zijazo. Tunahitaji watunga sera kuchukua hatua. Tunahitaji mashirika ya kiraia kuhamasishwa na sekta binafsi kuelewa kwamba kufanya chaguo bora zaidi leo kunamaanisha kufanya uwekezaji kuwa endelevu zaidi na wenye faida zaidi kwa kesho.”

Ingawa vipengele 120 vya hatua vinaweza kuonekana kuwa I vingi na vikubwa, Bwana Laborde amesisitiza kuwa lengo la mwisho ni kufikia "mabadiliko ya mfumo ambapo kila mtu anapaswa kuwa na jukumu".

FAO imezindua mpango wa kimataifa ili kutokomeza njaa ndani ya kiwango cha nyuzijoto 1.5 kinachohitajika
© FAO/Alessandro Penso
FAO imezindua mpango wa kimataifa ili kutokomeza njaa ndani ya kiwango cha nyuzijoto 1.5 kinachohitajika

Ni mwanzo mzuri 

Wakati huo huo, mchumi mkuu wa FAO, Maximo Torero, ameiambia Un News  kwamba lengo la mpango huu ni kubadilisha mifumo ya chakula cha kilimo kupitia hatua za asili za mabadiliko ya tabianchi ili "kusaidia kufikia uhakika wa chakula na lishe kwa wote, leo na kesho."

Kukiwa na takriban watu milioni 738 wenye utapiamlo duniani kote, Bwana. Torero amesema chakula lazima kiwe sehemu ya mjadala kuhusu hali ya hewa na lazima kuvutia uwekezaji wa hali ya hewa, ambao kwa sasa upo katika asilimia nne ambayo ni ndogo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa kuhusiana na mpango huo wa mwelekeo, FAO imesema fedha za mabadiliko ya tabianchi zinazoingia kwenye mifumo ya kilimo ni chini sana na zinaendelea kupungua ikilinganishwa na mtiririko wa fedha za hali ya hewa duniani, wakati ambapo aina hii ya ufadhili inahitajika haraka.

Amesema kazi inayofanywa katika COP28 ni "hatua nzuri ya kuanzia, na ramani hii inaweza kutoa mwongozo kwa ajili ya kutekeleza Azimio la Imarati kuhusu Kilimo endelevu, mifumo ya Chakula inayostahimili Kilimo, na hatua dhidi ya tabianchi, ambazo zilizinduliwa katika ufunguzi wa ngazi ya juu wa mkutano huu”.

Kuharakisha utekelezaji

Mpango huo wa FAO “ulizinduliwa katika siku maalum ya chakula, kilimo na maji katika jiji la maonesho la Dubai, ambapo mawaziri na maafisa wengine wakuu walikusanyika ili kujadili njia za kutekeleza Azimio la Imarati, ambalo sasa limetiwa saini na zaidi ya nchi wanachama 150.”

Katika ujumbe wake kwa hafla hiyo ya ngazi ya juu, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed alisema “Azimio hilo ni taarifa yenye nguvu ya dhamira ya kisiasa ya kuendesha mabadiliko tunayohitaji huku ukomo wa kufikia Ajenda ya 2030 ukikaribia kwa haraka.”

Ameendelea kusema kuwa "Ikiwa imesalia miaka saba kufikia malengo yetu ya maendeleo endelevu na mabadiliko ya tabianchi, tunahitaji kuimarisha kwa haraka juhudi zetu za pamoja kwa kutumia mifumo ya chakula kama njia ya kuharakisha utekelezaji."

Bi. Mohammed ameongeza kuwa njia yoyote ya kutimiza kikamilifu malengo ya muda mrefu ya Mkataba wa Paris lazima ijumuishe mifumo ya kilimo na chakula, ambayo zaidi ya theluthi moja ya hewa chafu hutoka.

Mapinduzi ya mwani

Suluhu moja la kibunifu kwa baadhi ya changamoto kubwa zaidi za kimataifa ambazo wanadamu wanakabili leo inaweza kupatikana katika mwani, "rasilimali kubwa zaidi tuliyo nayo kwenye sayari yetu ambayo hatujaitumia ipasavyo".

Hayo ni kwa mujibu wa Vincent Doumeizel, Mshauri Mwandamizi wa masuala ya bahari kwenye Mkataba wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa, ambaye ameiiambia timu ya UN News katika COP28 kwamba anaongoza "mapinduzi ya mwani ambayo yanaweza kusaidia kukabiliana na si tu mgogoro wa tabianchi, lakini pia uhakika wa chakula na migogoro ya kijamii.”

Bwana Doumeizel aliangazia uwezo mkubwa wa mwani wa kufyonza hewa ukaa na kuwa mbadala endelevu wa plastiki, na kuifanya kuwa zana nzuri ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na urejeshaji wa bayoanuwai.

Amesema "Mwani unaweza kukua haraka sana hadi sentimita 40 kwa siku hadi mita 60 juu. Kwa hivyo, mwani ni msitu halisi, na unavyonza hewa ukaa zaidi kuliko msitu wa Amazoni.”

Mashirika ya asasi za kiraia uyakiandamana kuhusu haki ya mabadiliko ya tabianchi kandoni mwa mkutano wa mabadiliko ya tabianchi Dubai
UNFCCC/Kiara Worth

Mtaalamu huyo wa bahari amesema mifumo ya chakula iliyopitwa na wakati ni miongoni mwa wachangiaji wakubwa wa mabadiliko ya tabianchi, upotevu wa viumbe hai, uhaba wa maji, kupungua kwa udongo na ukosefu wa haki za kijamii, pamoja na idadi kubwa ya watumwa wa kisasa wanaofanya kazi katika mifumo hii ya chakula".

Amesema kilimo cha mwani katika Afrika Mashariki tayari kimethibitisha uwezo wake wa kutengeneza ajira na kuwawezesha wanawake Afrika Mashariki ambapo "asilimia 80 ya mapato yanaenda kwa wanawake".

Bwana Doumeizel amebainisha kuwa licha ya kuwa na virutubisho na protini nyingi, karibu mwani wote mdogo sana tunaokula leo hukusanywa kwenye fuo.

Amesisitiza haja ya "kubadilisha simulizi ya hofu na maangamizi inayowasilishwa kwa vizazi vijavyo na kuwalisha matumaini na atarajio".

Amehitimisha kwa kusema kuwa “Ninaamini kwamba tukijifunza kulima bahari, tutakumbukwa kuwa kizazi cha kwanza duniani ambacho kitaweza kulisha watu wote huku tukikabiliana na mabadiliko ya tabianchi, huku tukirejesha viumbe hai na kupunguza umaskini. Tunaweza kukumbukwa hivyo, lakini inahitaji kukumbukwa kwa vyote kwa pamoja”.