Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walete walio hatarini ‘mbele ya mstari’ wa ufadhili wa tabianchi: COP28

Maafa yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi kama vile mafuriko, kama inavyoonyeshwa nchini Madagaska, yanaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya.
© UNICEF/Tsiory Andriantsoarana
Maafa yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi kama vile mafuriko, kama inavyoonyeshwa nchini Madagaska, yanaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya.

Walete walio hatarini ‘mbele ya mstari’ wa ufadhili wa tabianchi: COP28

Msaada wa Kibinadamu

Leo huko Dubai, UAE kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mazingira, COP28, Akaunti ya Hatua Dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi imezinduliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura (OCHA) ili kutoa njia ya ziada ya kufadhili hatua za kibinadamu kwenye majanga yanayohusiana na tabianchi kama vile mafuriko, ukame, dhoruba na joto kali, na kujenga uwezo wa kustahimili tabianchi. 

COP28 inaendelea Dubai, na ni dhahiri wadau wa mazingira na tabianchi wameshaona kuna athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi zinazoongeza machungu kwa wanadamu ambao wengine tayari wanakabiliwa na changamoto nyingine za kibinadamu. OCHA ambayo ni mdau muhimu wa misaada ya kibinadamu, pia ni sehemu muhimu ya Mfuko Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kukabiliana na Dharura (CERF), ambao kila mwaka, kati ya robo na theluthi ya ufadhili wake unaenda kwenye majanga yanayohusiana na tabianchi. 

Naibu wa Mkuu wa OCHA, Joyce Msuya amesisitiza umuhimu wa kuongeza ufadhili huu akisema "tunapoingia katika ulimwengu ambao mabadiliko ya tabianchi yanashikilia upanga juu ya kuongezeka kwa idadi ya watu". Jopo la serikali (duniani) kuhusu mabadiliko ya tabianchi IPCC, takribani watu bilioni 3.5, karibu nusu ya wanadamu wote duniani, wanaishi katika maeneo ambayo yanaweza kuathiriwa sana na mabadiliko ya tabianchi. 

Mwimbaji wa Senegal na rapa Oumy Gueye, anayejulikana kama OMG, ni miongoni mwa watetezi wa kibinadamu wanaotaka hatua zakukabiliana na tabianchi huko Dubai, Falme za Kiarabu, Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28).
UN News/Dominika Tomaszewska-Mortimer
Mwimbaji wa Senegal na rapa Oumy Gueye, anayejulikana kama OMG, ni miongoni mwa watetezi wa kibinadamu wanaotaka hatua zakukabiliana na tabianchi huko Dubai, Falme za Kiarabu, Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28).

Ili kusaidia nchi zilizo hatarini katika kujilinda na matokeo mabaya zaidi ya uharibifu wa tabianchi, mfuko wa hasara na uharibifu ulikubaliwa katika COP27 huko Sharm el-Sheikh mwaka jana na kuidhinishwa kuanza kutumika siku ya ufunguzi wa COP28 umesifiwa kama chombo muhimu cha haki ya tabianchi na. matokeo makubwa ya kwanza ya mkusanyiko huo unaoendelea hadi tarehe 10 mwezi huu. 

Zaidi ya dola milioni 650 zimeripotiwa kuahidiwa kufikia sasa na watetezi wa jamii zilizo katika mazingira magumu waliopo Dubai wamesisitiza haja ya kuhakikisha kwamba wale walioathirika zaidi wananufaika na ufadhili huo. 

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Filippo Grandi amesisitiz, "Sauti ya wale waliofurushwa na dharura hii lazima isikike, na lazima wajumuishwe katika mipango na ugawaji wa rasilimali.