Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP28

Mkutano wa 23 wa UN wa Mabadiliko ya Tabianchi: COP28
30 Novemba - 12 Desemba 2023: Dubai, Falme za Kiarabu

...

Viwango vya joto duniani vikiwa vimeongezeka na kuvunja rekodi, na matukio ya kupindukia ya hali ya hewa yakileta madhara kwa binadamu duniani kote, mwaka huu mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28, ni fursa ya kipekee ya kubadili mwelekeo na kuchochea hatua za kukabili janga la tabianchi.

COP28 ni pahala ambako dunia itatathmini utekelezaji wa Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya Tabianchi – mkataba wa aina yake uliopitishwa mwaka 2015 na kuweka mwelekeo wa kupunguza kwa kiasi kikubwa viwango vya utoaji wa hewa chafuzi ili kulinda uhai wa binadamu na mbinu za kujipatia kipato.

Wakuu wa Nchi, mawaziri na washauri na wasuluhishi, sambamba na wanaharakati wa tabianchi, mameya, wawakilishi wa mashirika ya kiraa na maafisa watendaji wakuu wa mashirika wanakutana kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Novemba huko Dubai, Falme za Kiarabu (UAE), ikiwa ni kusanyiko kubwa zaidi la mwaka kuhusu hatua kwa tabianchi.

Mabadiliko ya tabianchi yanachangia hali ya ukame katika maeneo mbalimbali duniani.
© WMO/Fouad Abdeladim

UDADAVUZI: COP28 ni nini, na kwa nini ni muhimu?

Hali ya joto duniani inaendelea kufikia viwango vya juu na kuvunja rekodi na, mwaka unavyofikia ukingoni, joto la kidiplomasia linaongezeka huku macho yote yakielekezwa Dubai, Falme za Kiarabu, ambako viongozi wa dunia wanakutana kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Desemba, ili kutathmini njia za kusonga mbele katika vita vya dunia dhidi ya mabadiliko tabianchi.