Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UDADAVUZI: COP28 ni nini, na kwa nini ni muhimu?

Mabadiliko ya tabianchi yanachangia hali ya ukame katika maeneo mbalimbali duniani.
© WMO/Fouad Abdeladim
Mabadiliko ya tabianchi yanachangia hali ya ukame katika maeneo mbalimbali duniani.

UDADAVUZI: COP28 ni nini, na kwa nini ni muhimu?

Tabianchi na mazingira

Hali ya joto duniani inaendelea kufikia viwango vya juu na kuvunja rekodi na, mwaka unavyofikia ukingoni, joto la kidiplomasia linaongezeka huku macho yote yakielekezwa Dubai, Falme za Kiarabu, ambako viongozi wa dunia wanakutana kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Desemba, ili kutathmini njia za kusonga mbele katika vita vya dunia dhidi ya mabadiliko tabianchi.

Hiki ndio unachopaswa kufahamu:

Mkutano wa mwisho wa COP ulifanyika Sharm El-Sheikh nchini Misri
United Nations/ Runa A
Mkutano wa mwisho wa COP ulifanyika Sharm El-Sheikh nchini Misri

'COP' ni nini?

Mikutano ya tabianchi ya Umoja wa Mataifa ni mikusanyiko mikubwa ya kila mwaka ya ngazi ya nchi inayojikita katika hatua za tabianchi, hujulikana kama COPs, Mkutano wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wa Mkataba wa  Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC).

Mkataba wa UNFCCC ulianza kutumika tarehe 21 mwezi Machi mwaka 1994 ili kuzuia binadamu kuvuruga mfumo wa tabianchi.

Leo, mkataba huo ulioridhiwa na nchi 198, inajumuisha wanachama wake wote duniani. Mkataba wa Parsi wa mabadiliko ya tabianchi uliopitishwa mwaka 2015, unafanya kazi kama nyongeza ya mkataba huo.

Zaidi ya watu 60,000 wanatarajiwa kushiriki COP28, wakiwemo wajumbe kutoka nchi wanachama wa UNFCCC, viongozi wa sekta, wanaharakati vijana, wawakilishi wa jamii za asili, waandishi wa habari, na wadau wengine.

Ni wakati muhimu kwa hatua dhidi ya tabianchi ulimwenguni.

COP28 itatupatia tathmini ya uhakika yaani kilele cha mchakato unaoitwa "Global Stocktake" au Kupitia yaliyofanyika duniani, ikimaanisha ni wapi ambapo dunia imefikia katika kukabiliana na janga la tabianchi na mabadiliko gani yanahitajika.

Wanafunzi wakipanda mikoko ili kama juhudi za kuwezesha ukanda wa pwani nchini Cambodia kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi
© UNDP/Manuth Buth
Wanafunzi wakipanda mikoko ili kama juhudi za kuwezesha ukanda wa pwani nchini Cambodia kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi

Kwa nini COP28 ni muhimu?

Tangu kupitishwa kwa Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi katika COP21 mwaka wa 2015, makongamano yaliyofuata yamejikita katika kutekeleza lengo lake kuu la kusitisha ongezeko la joto duniani hadi chini ya 2°C na kuendeleza juhudi za kupunguza ongezeko hilo hadi 1.5°C ya kabla zama za kuimarika kwa viwanda.

Ikiwa Paris ilitupa makubaliano, Katowice (COP24) na Glasgow (COP26) zilituonesha mpango huo, Sharm el-Sheikh (COP27) kisha ikatuhamisha kwenye utekelezaji.

Sasa, COP28 inatarajiwa kuwa hatua ya mageuzi, ambapo nchi hazikubaliani tu kwamba hatua kali zaidi za tabianchi zitachukuliwa bali pia kuonesha ‘JINSI’ ya kuzitekeleza.

 

Kupima maendeleo kuelekea kufikia malengo ya Paris juu ya kupunguza, kukabiliana na ufadhili wa tabianchi na kurekebisha mipango iliyopo ni sehemu muhimu ya fumbo, na hii ndiyo sababu COP28 inachukua umuhimu zaidi.

Uchambuzi wa kwanza wa jumla duniani COP26, ulioanza huko Glasgow, utakamilika huko Dubai.

Mchakato huo umeundwa ili kusaidia kutambua ni nini zaidi bado kinahitaji kufanywa na kuongoza nchi kuelekea mipango kabambe zaidi na ya kasi ya utekelezaji wa tabianchi.

Hivyo, uamuzi utakaofanywa na pande zinazoshiriki COP28 unaweza kuwa na matokeo muhimu zaidi baada ya mkutano wa Paris wa 2015.

Katibu Mkuu wa UN António Guterres (katikati) alipotembelea kituo cha Frei Antaktica, huko ncha ya kusini mwa dunia
UN Photo/Mark Garten
Katibu Mkuu wa UN António Guterres (katikati) alipotembelea kituo cha Frei Antaktica, huko ncha ya kusini mwa dunia

Ni nini kiko hatarini?

Ni kwamba afya ya sayari yetu na ustawi wa wanadamu.

"Barafu ya bahari ya Antaktika inaitwa ni jabalí lililolala, lakini sasa linaamshwa na zahma ya tabianchi," Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alionya wakati wa ziara yake huko kabla ya COP28.

Barafu ya bahari ya Antarctic imepungua sana, takwimu mpya zinaonesha kwamba Septemba mwaka  huu, ilikuwa na eneo la kilomita za mraba milioni 1.5 kiwango kidogo kuliko wastani wa kipindi hiki cha mwaka,  "eneo linalokaribia ukubwa wa Ureno, Hispania, Ufaransa na Ujerumani kwa pamoja".

"Haya yote yanaleta maafa kote ulimwenguni, kinachotokea Antaktika hakibaki Antaktika na kile kinachotokea umbali wa maelfu ya maili kina athari ya moja kwa moja hapa”, alisema.

Zaidi ya karne ya matumizi ya nishati ya kisukuku na matumizi yasiyo endelevu ya nishati na ardhi tayari yamesababisha ongezeko la joto duniani la 1.1°C juu ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda. 

Kila ongezeko la ongezeko la joto linaweza kuzidisha ukubwa na marudio ya matukio mabaya ya hali ya hewa kama vile mawimbi ya joto, mafuriko, dhoruba na mabadiliko tabianchi yasiyoweza kutenduliwa.

Mwaka wa 2023 unakaribia kuwa mwaka wa joto zaidi, wakati miaka minane iliyopita ikiwa ni miaka minane yenye joto zaidi kwenye rekodi ya dunia, ikiendeshwa na ongezeko la mkusanyiko wa gesi chafu na joto lililokusanyika.

Guterres ametoa tahadhari mara kadhaa kwa kuonya kwamba ikiwa hakuna kitakachobadilika, tunaelekea kwenye ongezeko la joto la 3°C, kuelekea ulimwengu hatari na usio na utulivu, “ubinadamu umefungua milango ya kuzimu joto la kutisha lina athari ya kutisha".

Takriban nusu ya watu duniani wanaishi katika maeneo ambayo yanaathiriwa na mabadiliko tabianchi.

Nchi zilizoendelea kidogo, zisizo na bahari na nchi ndogo za visiwa zinaweza kuwa zimechangia kidogo katika mzozo huu, lakini ndio wale wanaokabiliana moja kwa moja na matokeo yake mabaya.

Wanaharakati vijana wakitoa ujumbe wao kwa washiriki wa COP27 wakidai fidia kwa hasara na uharibifu kwa nchi maskini kutokana na jinsi zinaathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.
Kiara Worth
Wanaharakati vijana wakitoa ujumbe wao kwa washiriki wa COP27 wakidai fidia kwa hasara na uharibifu kwa nchi maskini kutokana na jinsi zinaathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.

Tunamaanisha nini kwa hatua kali dhidi  ya tabianchi?

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mara kwa mara amekuwa akitoa onyo kali kwamba dharura ya sasa wa hatua za tabianchi inalinganishwa na  ukubwa wa mgogoro huo, “lakini hatima haiku imara”.

Sayansi inaonesha wazi: bado inawezekana kupunguza ongezeko la joto hadi 1.5 ° C na kuepuka mabadiliko mabaya zaidi ya tabianchi, "lakini tu kwa hatua kubwa ya tabianchi za haraka na za moja kwa moja", ambazo ni pamoja na:

  • Kupungua kwa asilimia 45 kwa uzalishaji wa gesi chafu ifikapo mwaka 2030 ikilinganishwa na viwango vya 2010.
  • Kufikia uzalishaji wa sifuri duniani kote kufikia 2050
  • "Mpito wenye haki na sawa" kutoka kwa nishati ya fossa (mafuta na gesi) hadi vyanzo vya nishati mbadala.
  • Kuongezeka kwa uwekezaji katika kukabiliana na kustahimili uharibifu wa hali ya hewa
  • Lakini, kuna zaidi kama vile kutimiza ahadi za kifedha katika kuunga mkono nchi zinazoendelea, kupata dola bilioni 100 kwa mwaka kwa ajili ya  ufadhili wa kila mwaka wa tabianchi na kuendesha mfuko wa hasara na uharibifu, ambao ulikubaliwa mwaka jana katika COP27, kutoa haki kwa mabadiliko tabianchi.

Hata hivyo, ripoti ya awali ya muhktasari wa ahadi za kitaifa (NDCs) ya UNFCCC iliyotolewa mwezi Novemba inaonyesha kuwa dunia inashindwa kukabiliana na mgogoro wa mabadiliko tabianchi.

"Matamanio ya kimataifa yalidumaa katika mwaka uliopita na mipango ya kitaifa ya tabianchi inakinzana sana na sayansi,", alisema Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa.

Dubai, mji ulioko Falme za Kiarabu ndio mwenyeji wa COP28
© Unsplash/Lucy M
Dubai, mji ulioko Falme za Kiarabu ndio mwenyeji wa COP28

Je, nini jukumu Umoja wa Falme za Kiarabu, kama mwenyeji wa COP28?

Mikutano ya tabianchi ya Umoja wa Mataifa huandaliwa na nchi tofauti kila mwaka, mwaka huu, Umoja wa Falme za Kiarabu ni mwenyeji wa mkutano wa kilele wa COP28 kati ya tarehe 30 Novemba na 12 Desemba.

Mwenyeji pia huteua rais ambaye anaongoza mazungumzo ya tabianchi na kutoa uongozi na maono ya jumla.

Waziri wa Viwanda na Teknolojia ya Juu wa UAE Dkt. Sultan al-Jaber, ndiye atakuwa Rais wa COP28.

Rais anayekuja ameeleza mkazo wake mkuu katika mabadiliko katika maeneo manne muhimu:

  • Kuongeza kasi ya mpito wa nishati na kupunguza uzalishaji kabla ya 2030
  • Kubadilisha fedha za tabianchi, kwa kutimiza ahadi za zamani na kuweka mfumo wa mpango mpya
  • Kuweka asili, watu, maisha, na riziki katika moyo wa hatua ya tabianchi.
  • Kuhamasisha kwa ajili ya COP iliyojumuisha zaidi kuwahi kutokea
Meli ya kuchimba mafuta baharini ikiwa kando ya pwani ya Magharibi mwa Marekani
© Unsplash/Arvind Vallabh
Meli ya kuchimba mafuta baharini ikiwa kando ya pwani ya Magharibi mwa Marekani

COP28 itachangiaje katika vita vya dunia dhidi ya mabadiliko tabianchi.

Takribani miaka minane baada ya Makubaliano ya Paris na nusu ya njia kuelekea Ajenda ya 2030, COP28 ni fursa inayofaa ya kuanza njia mpya kuelekea hatua za tabianchi zilizo na ufanisi.

Kama ripoti kadhaa za Umoja wa Mataifa zinavyoonyesha, dunia haiko kwenye njia ya kufikia malengo ya Mkataba wa Paris, lakini matumaini ni kwamba serikali katika COP28 zitaweka ramani ya kuharakisha hatua za tabianchi.

Mnamo 2020, nchi moja moja zilikuja na mipango ya kitaifa ya utekelezaji wa tabianchi inayolenga kupunguza uzalishaji wa hewa chafu kitaifa na kukabiliana na athari za mabadiliko tabianchi.

Kwa awamu inayofuata ya mipango hii iliyopangwa kwa 2025, matokeo ya uchambuzi wa jumla yanaweza kuhamasisha nchi kuongeza uamuzi na kuweka malengo mapya, yakizidi sera na ahadi zilizopita.

Kwa mengine yanayoshikiliwa, mkutano wa Dubai ni wakati madhubuti wa kugeuza mipango ya tabianchi kuwa hatua kali na kubadili mwelekeo dhidi ya mgogoro wa tabianchi.