Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP28

Mkutano wa 23 wa UN wa Mabadiliko ya Tabianchi: COP28
30 Novemba - 12 Desemba 2023: Dubai, Falme za Kiarabu

...

Viwango vya joto duniani vikiwa vimeongezeka na kuvunja rekodi, na matukio ya kupindukia ya hali ya hewa yakileta madhara kwa binadamu duniani kote, mwaka huu mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28, ni fursa ya kipekee ya kubadili mwelekeo na kuchochea hatua za kukabili janga la tabianchi.

COP28 ni pahala ambako dunia itatathmini utekelezaji wa Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya Tabianchi – mkataba wa aina yake uliopitishwa mwaka 2015 na kuweka mwelekeo wa kupunguza kwa kiasi kikubwa viwango vya utoaji wa hewa chafuzi ili kulinda uhai wa binadamu na mbinu za kujipatia kipato.

Wakuu wa Nchi, mawaziri na washauri na wasuluhishi, sambamba na wanaharakati wa tabianchi, mameya, wawakilishi wa mashirika ya kiraa na maafisa watendaji wakuu wa mashirika wanakutana kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Novemba huko Dubai, Falme za Kiarabu (UAE), ikiwa ni kusanyiko kubwa zaidi la mwaka kuhusu hatua kwa tabianchi.

COP28

Solar Sister watekeleza kwa vitendo nishati safi kwa jamii za pembezoni

Kila uchao, sauti zinapazwa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, tena hasa wakati huu ambapo wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC wakikutana Dubai, huko Falme za Kiarabu kwenye mkutano wao wa 28 au COP28. Tayari  hatua zimechukuliwa na shirika la kimataifa la Solar Sister kusaka nishati salama hasa kwa wanawake wa vijijini kama anavyoshuhudia mwanachama na mnufaika wake, Loveness Sabaya wa jamii ya kimasai kutoka Arusha nchini Tanzania kupitia video iliyochapishwa kwenye ukurasa wa X wa mkutano wa COP28. 

Sauti
1'39"