Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP28

Mkutano wa 23 wa UN wa Mabadiliko ya Tabianchi: COP28
30 Novemba - 12 Desemba 2023: Dubai, Falme za Kiarabu

...

Viwango vya joto duniani vikiwa vimeongezeka na kuvunja rekodi, na matukio ya kupindukia ya hali ya hewa yakileta madhara kwa binadamu duniani kote, mwaka huu mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28, ni fursa ya kipekee ya kubadili mwelekeo na kuchochea hatua za kukabili janga la tabianchi.

COP28 ni pahala ambako dunia itatathmini utekelezaji wa Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya Tabianchi – mkataba wa aina yake uliopitishwa mwaka 2015 na kuweka mwelekeo wa kupunguza kwa kiasi kikubwa viwango vya utoaji wa hewa chafuzi ili kulinda uhai wa binadamu na mbinu za kujipatia kipato.

Wakuu wa Nchi, mawaziri na washauri na wasuluhishi, sambamba na wanaharakati wa tabianchi, mameya, wawakilishi wa mashirika ya kiraa na maafisa watendaji wakuu wa mashirika wanakutana kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Novemba huko Dubai, Falme za Kiarabu (UAE), ikiwa ni kusanyiko kubwa zaidi la mwaka kuhusu hatua kwa tabianchi.

01 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunaangazia mabadiliko ya tabianchi na malelengo ya maendeleo endelevu kupitia mchezo wa mpira wa miguu. Makala tutaelekea nchini DRC kusikia simulizi ya wakimbizi na mashinani tunakupeleka nchini Tanzania kusikia ni kwa vipi wanawake wameweza kufanya kazi zao na kunyonyesha watoto wao ipasavyo.

Sauti
12'14"
Sio tu kwamba mikoko inasaidia kuzuia kuendelea kwa mabadiliko ya tabianchi, lakini pia ina jukumu muhimu katika kupunguza athari zake.
The Mangrove Photography Awards/Shyjith Kannur

Haya ndiyo mambo ya kutarajia katika Wiki ya mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi barani Afrika 2023

Viongozi wa Afrika wanatarajiwa kukutana jijini Nairobi, kenya wiki ijayo kwa jaili ya wiki ya mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi, Mkutano wa kila mwaka ambao wanatarajiwa kujadili njia mbalimbali za kupunguza utoaji wa gesi chafuzi huku wakija na mbinu za mnepo wa kukabiliana na athari za hali ya hewa.