Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

UM wasikitishwa na kifo cha muhamiaji toka Angola

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu za wahamiaji Jorge Bustamante na kundi maalumu la kuangalia matumizi ya askari mamluki leo wamesema wanatiwa hofu na taarifa za kifo cha abiria mmoja aliyekuwa akirejeshwa kwa nguvu Angola kutoka Uingereza.

Waathirika wa uhalifu wapatie msaada:Cage

Kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa dhidi ya uhalifu wa kupangwa mjini Vienna Austria mtayarishaji na mcheza filamu mashuhuri ambaye ni mshindi wa tuzo ya Oscar na balozi mwema wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na uhalifu na mihadarati UNODC, Nicolas Cage leo amesisitiza nia yake ya kuwasaidia maelfu ya wanawake na watoto ambao maisha yao yameathirika na uhalifu.

UM waongeza ndege kusafirisha vifaa vya kura ya amaoni Sudan

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan kimeongeza ndege nane zaidi na kufikisha idadi yote ya ndege zake kuwa 24 zitakazosaida kusafirisha tani 120 za vifaa vitakavyotumiwa kwenye kura ya maoni Januari mwakani itayoamua iwapo Sudan Kusini itakuwa huru kutoka sehemu zingine za nchi.