Skip to main content

Kampeni za uchaguzi wa Urais Ivory Coast zimeanza vyema:UM

Kampeni za uchaguzi wa Urais Ivory Coast zimeanza vyema:UM

Kampeni za uchaguzi wa raia uliocheleweshwa sana nchi Ivory Coast hatimaye zimeanza kwa amani na utulivu.

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Young-jin Choi amesema uchaguzi huo unatarajiwa kumaliza mgawanyiko katika nchi hiyo ya Arika ya Magharibi, uliosababishwa na vita vya wenye kwa wenyewe vya mwaka 2002.

Bwana Choi amesema anafuraha licha ya matatizo yaliyopo kuona changamoto kubwa ya kusafirisha vitambulisho na kadi za wapiga kura imekamilika. Ameyasema hayo baada ya kukutana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa nchi hiyo mjini Abidjan. Jayson Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)