Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukraine

Ukraine

Martin Griffiths, Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, akihutubia Baraza la Usalama kwa njia ya video kuhusu amani na usalama nchini Ukraine
Picha ya UN /Eskinder Debebe

“Ni dhahiri kwamba watu wa Ukraine na mamilioni ya wengine kote duniani hawawezi tena kumudu kuendelea kwa vita hii. Sasa kuliko wakati mwingine wowote ule wanahitaji kukomeshwa kwa uhasama na suluhu ya kisiasa ipatikane ili kumaliza vita."

Mkuu wa OCHA, Martin Griffiths  akihutubia Baraza la Usalama, New York, Marekani, 15 Mei 2023.

MAELEZO YA JUMLA

Hali ya usalama nchini Ukraine ilizorota haraka kufuatia hatua ya Urusi kuanza operesheni ya kijeshi tarehe 24 mwezi Februari mwaka 2022. Mashambulizi hayo yalienea katika mikoa minane, ikiwemo Kyviska, Oblast na mji mkuu Kyiv pamoja na maeneo ya mashariki ya Donetsk na Luhanks ambako tayari yalikuwa yamegubikwa na mizozo.

Kusambaa kwa mzozo kumechochea ongezeko la haraka la mahitaij ya kibiinadamu kwa kuwa huduma za msingi zimevurugwa na raia wanakimbia. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa takribani watu milioni 12 walioko Ukraine wanahitaji ulinzi na misaada, ilhali wengine milioni 4 ambao ni wakimbizi watahitaji misaada ya ulinzi na mingineyo katika nchi jirani kwa kipindi kijacho.

Tarehe 1 mwezi Machi mwaka 2022, Umoja wa Mataifa na wadau wa  maendeleo walizindua ombi liliroratibiwa la pamoja la haraka la dola bilioni 1.7 ili kupelekea misaada ya dharura ya kibinadmu kwa wananchi wa Ukraine walioko ndani ya nchi hiyo na waliokimbilia nchi jirani.

Ndani ya Ukraine, mpango huo unahitaji dola bilioni 1.1 ili kukidhi mahtaji ya haraka ya kibinadamu ya watu milioni zaidi ya 6 walioathirika na waliofurushwa makwao kutokana na operesheni za kijeshi. Fedha hizo ni kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo/ Nje ya Ukraine, UN inaomba dola milioni 551 kusaidia raia wa Ukraine waliosaka hifadhi huko Poland, Hungary, Romania na Moldova.

Amin Awad, Mrartibu wa UN wa janga la sasa huko Ukraine ametaka sitisho la haraka hla mapigano ili misaada ya kibinadamu iweze kusambazwa.  Ametoa kauli hiyo tarehe 5 mwezi Machi wakati mapigano kati ya majeshi ya Urusi na Ukraine yakiendelea huku misaada ya UN ikiendelea kuwasili nchini humo.

Pata taarifa k uhusu timu ya UN nchini Ukraine hapa.

YALIYOMO

Wakati machafuko yakishika kasi Ukraine watu wamesongamana kwenye kituo cha tren Lviv wakisubiri kusafirishwa kwenda Poland
Wakati machafuko yakishika kasi Ukraine watu wamesongamana kwenye kituo cha tren Lviv wakisubiri kusafirishwa kwenda Poland, by © UNICEF/Aleksey Filippov

UN yashtushwa na athari za kibinadamu katika miji iliyozingirwa Ukraine

Katika siku ya 24 ya mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine, na wakati mapigano yakizidi, haswa katika miji ya Mariupol, Sumy, Kharkiv, Chernihiv, Sievierodonetsk na kaskazini mwa Kyiv, mashirika ya kibinadamu yameelezea wasiwasi wao mkubwa juu ya hatima ya raia walionaswa katika miji iliyozingirwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), mashambulizi yanayolengwa dhidi ya raia na miundombinu ya kiraia na ukosefu wa njia salama za kuondoka yanaongeza hatari na kutishia maisha ya maelfu ya raia.

"Ripoti za kibinadamu zilizopokelewa kutoka maeneo haya ni za kutisha, na tunaendelea kutoa wito wa ulinzi wa raia na miundombinu ya kiraia, na kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa za kibinadamu," amesema Matthew Saltmarsh, msemaji wa UNHCR mjini Geneva Uswis.

Soma habari kamili

Katibu Mkuu wa UN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kwenye mimbali0 akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu Ukraine. (Picha ya Maktaba)
UN Photo/Manuel Elías

Ujumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uko dhahiri: Malizeni chuki Ukraine — sasa. Wekeni silaha chini — sasa. Fungueni milango ya mazungumzo na diplomasia — sasa.  
Hatuna muda wa kupoteza. Madhara ya kikatili ya mapigano yako dhahiri. Lakini licha ya hali mbayá ya wananchi wa Ukraine hivi sasa, inatisha kuona hali itakuwa mbayá zaidi. Saa inasonga na janga litalipuka.
Dunia inataka kumaliza machungu ya kibinadamu Ukraine. Ukweli huu huu ulikuwa wazi katika hamasisho la haraka la kupata fedha za kusaidia operesheni za kibinadamu Ukraine na nchi jirani. Ombi letu la dharura lilitimizwa kwa ukarimu mkubwa.
Kuangalia mbele, nitaendelea kufanya kila niwezalo katika uwezo wangu kuchangia katika sitisho la haraka la chuki na kuwepo kwa mashauriano ya kuleta amani. Wananchi wa Ukraine wanahaha kupata amani. Na watu kote duniani wanadai hilo.

Soma hotuba nzima hapa

 
Amin Awad, UN Assistant Secretary-General Crisis Coordinator for Ukraine.

Mratibu wa UN wa Janga la Ukraine

Amin Awad kutoka Sudan, ameteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa Msaidizi wake wa  na kuhudumu kama  Mratibu wa UN wa Janga la Ukraine.

Baraza la Usalama la UN
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likiwa katika mkutano wa dharura kuhusu Ukraine.
UN Photo/Evan Schneider

Tarehe 31 mwezi Januari mwaka 2022, Baraza la Usalama lilikutana kufuatia ombi la Marekani kuhusu ripoti ya kwamba Urusi imepeleka zaidi ya askari 100,000 na vifaa vya vita kwenye mpaka wa Urusi na Ukraine.

Jumatatu ya tarehe 21 mwezi Februari mwaka 2022, Baraza lilikutana katika kikao cha dharura, kwa ombi la ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu wa Ukraine juu ya uamuzi wa Urusi wa kutambua baadhi ya maeneo ya majimbo ya Ukraine ya Donetsk na Luhansk kama maeneo huru. Mkuu wa Idara ya Siasa ya Umoja wa Mataifa Rosemary DiCarlo, akihutubia Baraza la Usalama aliibua hofu juu ya matumizi ya neno “ujumbe wa kulinda amani”  iliyotumiwa na Urusi na pia akaonya kuhusu hatari ya kikanda na kimataifa.

Kikao hicho cha dharura kilifuatiwa na vikao vingine vitatu tarehe 23, 25 na 27 Februari. Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, katika taarifa yake fupi wakati wa kikao cha usiku wa tarehe 23 Machi, alimsihi kwa dhati Rais Vladmir Putin wa Urusi azuie majeshi yake yasishambulie Ukraine. Hata hivyo dakika chache baada ya wito huo, ripoti ziliibuka kuwa Urusi imeanza operesheni maalum ya kijeshi ndani ya Ukraine. Wajumbe kadhaa wa Baraza walilaani mwendelezo huo.

Jioni ya Ijumaa ya tarehe 25 Februari 2022, katika jibu lake kufuatia shambulizi la Urusi, Baraza lilikutana tena kupigia kura azimio lililoandaliwa na Marekani na Albania na kuungwa mkono na nchi kadhaa wanachama, azimio ambalo lilikuwa linalaani uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine na kutoa wito kwa Urusi kuondoa majeshi  yake. Nchi 11 wanachama wa Baraza waliunga mkono azimio, nchi 3, (China, India na Falme za Kiarabu) hazikupiga kura kabisa, ilhali Urusi ambayo ilikuwa inashikilia urais wa Baraza kwa mwezi Februari ilipiga kura turufu kupinga azimio hilo.

Jumapili ya tarehe 27 mwezi Februari, 2022, kwa mara ya nne ndani ya wiki moja, Baraza lilikutana tena katika kikao cha dharura na kupitisha kanuni ya utekelezaji- ijulikanayo rasmi kama ‘Kuungana kwa ajili ya amani’ – na kutoa wito kwa Baraza Kuu la UN lenye wanachama 193 lichukue hatua ya dharura na kuandaa azimio amalo litataka kusitishwa haraka kwa operesheni za kijeshi za Urusi nchini Ukraine.

Habari za UN News kutoka Baraza la Usalama kuhusu Ukraine

Baraza Kuu la UN
Matokeo ya kura ya azimio kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Ukraine
UN

Kadri hali ya usalama barani Ulaya ilivyozidi kudorora kufuatia operesheni za kijeshi za Urusi dhidi ya Ukraine, Urusi tarehe 26 mwezi Februari ilipiga kura turufu dhidi ya azimio la Baraza la Usalama la kulaani na kusitisha uvamizi wa Ukraine. Kura ya HAPANA k utoka kwa mjumbe yeyote wa kudumu kwenye Baraza hilo, ambazo ni China, Urusi, Uingereza, Marekani na Ufaransa, humaanisha kuwa hatua haiwezi kupitishwa.

Mwishoni mwa mkutano Barazani, Ukraine na wajumbe wengine kadhaa waliahidi kuwasilisha azimio kama hilo ndani ya Baraza Kuu ambako humo hakuna kura turufu.

Jumapili ya tarehe 27 mwezi Februari 2022, Baraza la Usalama liliitisha kikao cha dharura na kupitisha kanuni ya utekelezaji- ijulikanayo rasmi kama ‘Kuungana kwa ajili ya amani’ – na kutoa wito kwa Baraza Kuu la UN lenye wanachama 193 lichukue hatua ya dharura na kuandaa azimio ambalo litataka kusitishwa haraka kwa operesheni za kijeshi za Urusi nchini Ukraine. 

Chini ya kanuni hiyo ya Kuungana kwa ajili ya Amani, Baraza lina uwezo wa kuchukua hatua iwapo Baraza la Usalama kwa sababu ya kukosa makubaliano baina ya nchi zenye ujumbe wa kudumu, linashindwa kutekeleza jukumu lake kuu la wajibu wa kuchukua hatua zinazotakiwa kulinda amani na usalama duniani.

Baraza liliitisha mkutano wa dharura wa 11 tarehe 1 Machi 2022 na baada ya hotuba kutoka kwa nchi wanchama, wajumbe wengi walipitisha azimio tarehe 2 Machi 2022 la kutaka Urusi iondoe majeshi yake nchini Ukraine.

Jumla ya kura 141 ziliunga mkono azimio ambalo linasisitiza mamlaka na uhuru wa Ukraine kwa utambuzi wa mipaka yake inayotambuliwa kimataifa.

Mashirika ya UN

Mashirika ya UN nchini Ukraine

Mnamo tarehe 25 Februari 2022, watu walijificha shuleni wakati wa operesheni za kijeshi zinazoendelea huko Kyiv, Ukraine.
© UNICEF/Victor Kovalchuk/UNIAN
Mnamo tarehe 25 Februari 2022, watu walijificha shuleni wakati wa operesheni za kijeshi zinazoendelea huko Kyiv, Ukraine.
Dinu Lipcanu, Head of UNHCR's Mariupol field office in Ukraine, visits local residents whose houses have been damaged by artillery shelling in Avdiivka, Donetsk. (file)
UNHCR | Operational Data Portal
Mama akiwa ame,mbeba binti yake katika nyumba yao iliyoko karibu kabisa na msitari wa makabiliano Ukraine (Toka Maktaba)
OCHA
Mnamo tarehe 27 Februari 2022, halijoto ikiwa karibu na nyuzi joto sifuri Selcius, mtoto aliyevikwa blanketi anajiweka joto wakati yeye na familia yake wakisubiri kupanda treni ya uokoaji huko Lviv, kona ya magharibi kabisa ya Ukraine
UNICEF
Shehena ya biskuti zenye nishati nyingi kwa ajili ya wakimbizi wa Ukraine inapakuliwa katika uwanja wa ndege nchini Poland.
WFP
Watoto hutunzwa katika kituo cha uzazi cha muda kilicho chini ya jengo la matibabu huko Saltivka, huko Kharkiv, Ukraine.
UNFPA
Mma Mzee wa kijiji cha Krymskoe, apewa msaada wa fedha na IOM.
UNDP
Mtoto aliyeshikwa na babaye na Muuguzi anampa shindano ya  kwanza ya Surua, matubwitubwi na rubella.
WHO
Picha ya kiwanda cha nyuklia cha Chernobyl baada ya ajali.
IAEA
 

 

VIDEO NA SAUTI KUHUSU UKRAINE