Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wasikitishwa na kifo cha muhamiaji toka Angola

UM wasikitishwa na kifo cha muhamiaji toka Angola

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu za wahamiaji Jorge Bustamante na kundi maalumu la kuangalia matumizi ya askari mamluki leo wamesema wanatiwa hofu na taarifa za kifo cha abiria mmoja aliyekuwa akirejeshwa kwa nguvu Angola kutoka Uingereza.

Bwana Mubenga alikuwa ameketi katika kiti cha nyuma akizungukwa na walinzi watatu wa kampuni ya G4S. Kwa mujibu wa mashahidi waliwaona walinzi hao wakimkandamiza huku akilalamika hawezi kupumua na kuomba msaada kwa abiria wengine.

Bwana Bustamante amesema inasikitisha kuona jinsi wanavyotendewa wahamiaji bila utu, kutokana na kuwachukulia kama wahalifu. Ameongeza kuwa anazikumbusha serikali, makampuni binafsi na sekta za umma kuzingatia haja ya kuwachukulia wahamiaji kama binadamu kwa utu na hkuheshimu haki zao.