Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

UM wazingatia machafuko katika Usomali

UM umeripoti ya kuwa mfumko wa mapigano yaliojiri karibuni Usomali ni tukio liliosababisha uharibifu mkubwa kihali na mali ambapo mamia ya watu walijeruhiwa na idadi isiyojulikana ya maututi walionyimwa maisha baada ya kujikuta katikati ya mashambulio baina ya vikosi vya Serekali ya Mpito (TFG) na kundi la Umoja wa Mahakama za Kiislamu (UIC).

UNICEF yatangaza ombi la misaada ya kuhudumia Chad

Shirika la UM juu ya Maendeleo ya Watoto (UNICEF) wiki hii limetangaza ombi maalumu lenye kuwahimiza wahisani wa kimataifa kufadhilia msaada wa dharura wa dola milioni 9 kukidhia mahitaji ya mamia elfu ya wahamiaji waliopo kwenye maeneo ya mashariki na kusini ya Chad.

Hapa na pale.

KM mpya wa UM, Ban Ki-moon anatazamiwa kuanza kazi rasmi mnamo Ijumanne, tarehe 02 Januari 2007. ~

Mkutano wa kuaga, Katibu Mkuu na waandishi habari wa kimataifa

Ijumanne KM Kofi Annan alikuwa na mahojiano ya mwisho, ya kuaga, na waandishi habari wa kimataifa wanaofanya kazi kwenye Makao Makuu ya UM mjini New York. Mwanadiplomasiya wa nambari ya kwanza Annan alikiri kwenye risala yake kwamba kutofanikiwa kuzuia vita na uvamizi wa Iraq lilikuwa ni tukio moja liliomhuzunisha sana kabisa katika miaka 10 aliyoitumikia taasisi hii ya kimataifa.

Ripoti ya UNICEF yalaani 'utalii wa hasharati' katika mwambao wa Kenya

Ripoti ya UNICEF iliyozingatia masuala yanayoambatana na kile kinachotambuliwa kama \'utalii wa uasherati\' katika Kenya imefichua ya kwamba karibu asilimia 30 ya vijana wa kike, ikijumuisha vijana 10,000 hadi 15,000 katika maeneo ya mwambao ya Malindi, Mombasa, Kilifi na Diani hushiriki kwenye vitendo karaha vya ukahaba na umalaya.

Muhtasari wa matukio katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Kikao cha 61 cha Baraza Kuu la UM kinajongelea kukamilisha mijadala yake ambapo ripoti za mijadala ya zile zile kamati zake sita kuhusu masuala ya usalama, maendeleo ya uchumi na jamii, sheria ya kimataifa na bajeti la UM, ziliwakilishwa mbele ya Baraza Kuu kupigiwa kura na wajumbe wa kimataifa.

Burundi itahitajia msaada wa kimataifa kujenga amani, yasema UM

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Burundi, Nureldin Satti aliwaambia waandishi habari wa kimataifa katika Makao Makuu ya kwamba licha ya kuwa Shirika la Ulinzi wa Amani la UM katika Burundi (ONUB) litamaliza operesheni zake mwisho wa mwezi Disemba hatua hiyo haimaanishi mchango wa kimataifa hauhitajiki tena.

Mahakama ya ICTR yataka hukumu ya Seromba irekibishwe

Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) amependekeza hukumu ya kifungo cha miaka 15 aliopewa Athanase Seromba karibuni ibadilishwe kwa sababu anaamini mtuhumiwa huyo aliyekuwa padri wa Parokia ya Nyange, katika kijiji cha Kivumu alishiriki kwenye makosa ya jinai ya hali ya juu iliyohusika na mauaji ya halaiki. Kwa hivyo, Mwendesha Mashitaka angelipendelea Seromba anapewa adhabu kali zaidi.