Waathirika wa uhalifu wapatie msaada:Cage
Kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa dhidi ya uhalifu wa kupangwa mjini Vienna Austria mtayarishaji na mcheza filamu mashuhuri ambaye ni mshindi wa tuzo ya Oscar na balozi mwema wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na uhalifu na mihadarati UNODC, Nicolas Cage leo amesisitiza nia yake ya kuwasaidia maelfu ya wanawake na watoto ambao maisha yao yameathirika na uhalifu.
Bwana Cage ametoa wito kwa niaba ya waathirika hao wasio na hatia kwenye mkutano huo wa Umoja wa Mataifa ambao unatathimini hatua zilizopigwa muongo mmoja baada ya kuridhiwa kwa mkataba wa kupinga uhalifu wa kupangwa wa kimataifa. Cage amesema katika harakati zake kama balozi mwema wa Umoja wa Mataifa amekutana na waathirika wengi sana na kusikitishwa na hadhithi zao.
(SAUTI YA NICOLAS CAGE)
Naye mkurugenzi mkuu wa UNODC Yur Fedotov amepongeza juhudi za Nocolas Cage za kujidhatiti kuwasaidia waathirika wa uhalifu wa kupangwa. Amesema Cage alianzisha mfuko kuwasaidia watoto waliokuwa askari zamani kwa kuwapatia malazi, huduma za afya na ushauri nasaha, pia kwa kuisaidia UNODC ameunga mkono juhudi za kimataifa za kudhibitti silaha, na ujenzi mpya wa New Orleans baada ya kimbunga Katrina.