Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zihudhurie mkutano wa kutokomeza mabomu ya vishada:Migiro

Nchi zihudhurie mkutano wa kutokomeza mabomu ya vishada:Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro amesema ni muhimu kwa mataifa yote duniani kuhudhuria mkutano ujao wa kukabiliana na mabomu ya vishada ili kuleta uhalisia wa utekelezaji mkataba wake.

Bi Migoro pia amezitolea mwito nchi ambazo bado hazijasaini mkaba huo zichukue fursa ya kuhudhuria mkutano huo ambao mkataba wake umeanza kufanya kazi Agust 1 mwaka huu ikiwa ni miaka miwili tangu kuarisiwa kwake.

Naibu Katibu Mkuu hata hivyo amesifu juhudi zinazofanywa na taasisi za kiraia ambazo zimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba mkataba huo siyo tu unaungwa mkono lakini pia unatekelezwa.

Mabomu hayo ya vishada kwa mara ya kwanza yalianza kutumika wakati wa vita vya kwanza vya dunia na yameendelea kuangamiza mamia ya watu duniani kote.