Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kurejea ndani ya Somalia baada ya miaka 17

UM kurejea ndani ya Somalia baada ya miaka 17

Umoja wa Mataifa unajiandaa kujerea kikamilifu ndani ya Somalia kuanzisha uwepo wa kisia kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 17 kwa eengo la kuunda katiba mpya na serikali .

Akizungumza mjini New York mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini Somalia Dr Augustine Mahiga amesema kubwa zaidi ni kuzuia magaidi wasichukue serikali. Somalia imekuwa bila serikali kuu kwa zaidi ya miongo miwili sasa, Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Umoja wa Mataifa unapanga mikakati ya kupeleka wafanyikazi wanne kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu na wengine watano katika maeneo yanayojitawala ya Puntland na Somaliland. Mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga amesema kuwa Umoja wa Mataifa utahamisha ofisi zake za kisiasa kutoka Nairobi kwenda Somalia.

Mahiga anasema kuwa ni jambo muhimu kuwa na wafanyikazi wa kimataifa nchini Somalia wanaoweza kushauriana na serikali ya mpito , wazee na viongozi wa kidini. Anasema kuwa Umoja wa Mataifa utakuwa na jukumu la kutafuta makubaliano na mipango ya kubuniwa kwa serikali itakayochukua mahala pa serikali ya mpito ambayo wakati wake wa kuhudumu utakamilika mwezi Agosti mwak 2011.

 Mahiga ameongeza kuwa UM unahitaji kubuni wizara katika nyanja za ulinzi , uchumi, afya , elimu na mawasiliano. Eneo kubwa la kusini na kati kati mwa Somalia linadhibitiwa na kundi la wanamgambo la al-Shabaab walio na mafungamano na kundi la kigaidi la al-Qaeda.