Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MINUCART inajiandaa kuondoka nchini Chad

MINUCART inajiandaa kuondoka nchini Chad

Mpango wa kulinfda amani wa Umoja wa Mataifa nchi Jamuhuri ya Afrika ya Kati na Chad MINUCART unajiandaa kuondoka nchini Chad.

MINUCART imeanza kukabidhi majukumu ya ulinzi na usalama kwa vikosi vya serikali ya Chad ambavyo vitatwaa rasmi jukumu hilo mwishoni mwa mwaka huu wakati askari wa MINUCART watakapoondoka. Serikali ya Chad iliuomba Umoja wa Mataifa mapema mwaka huu kuondoa vikosi vyake na kukabidhi jukumu la ulinzi na usalama kwa serikali ya nchi hiyo. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Mkuu wa vikosi hivyo vya Umoja wa Mataifa ambavyo pia vinafanya kazi huko Afrika ya Kati, MINURCAT Bwana Youssef Mahmoud amesema kuwa kazi ya kuwafunza askari wazalendo imekuwa ikiendelea hadi sasa.

Tayari mpango wa utoaji mafunzo umewafaidia askari kadhaa na wengine 200 wameanza kupata mafunzo hayo ya kuchukua majukumu ya ulinzi wa amani. Inakadiriwa kuwa hadi kufikia mwisho askari 1,000 watakuwa wamepatiwa mafunzo hayo.

Kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa MINURCAT kilipelekwa kwenye eneo hilo ili kuwalinda raia na kuendesha shughuli za utoaji misaada ya usamaria wema kufuatia kukosekana kwa utengamao wa amani baina ya mataifa hayo mawili na kuongezeka kwa hali tete toka nchi jirani ya Sudan.