Skip to main content

UM waongeza ndege kusafirisha vifaa vya kura ya amaoni Sudan

UM waongeza ndege kusafirisha vifaa vya kura ya amaoni Sudan

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan kimeongeza ndege nane zaidi na kufikisha idadi yote ya ndege zake kuwa 24 zitakazosaida kusafirisha tani 120 za vifaa vitakavyotumiwa kwenye kura ya maoni Januari mwakani itayoamua iwapo Sudan Kusini itakuwa huru kutoka sehemu zingine za nchi.

Mratibu wa ujumbe wa UM kusini mwa Sudan UNMIS David Gressly amesema kuwa ndege zaidi zitaongezwa ili kukabiliana na changamoto za kufika katika vituo vya kupigia kura na vya kujiandikisha vilivyo maeneo ya vijijini yaliyo mbali vitakavyobuniwa ifikapo Januari mwakani.

Kura mbili za maoni zinatarajiwa kuandaliwa ya kwanza ikiwa ni awamu ya mwisho ya kutekelezwa kwa makubaliono ya mwaka 2005 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miongo miwili ya kuamua iwapo sudan kusini itakuwa huru na ya pili ikiandaliwa katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Abyei ya kuamua ikiwa eneo hilo litajiunga na kaskazini au kusini.