Burundi

Mama mkimbizi kutoka Burundi akiwa na watoto wake kambini nchini Tanzania. Picha: UNHCR
Upungufu wa fedha za kufadhili miradi ya kuwasaidia wakimbizi hao imesababisha wengi kuendelea kuishi katika mahema ya dharura wengine tangu miaka miwili iliyopita walipowasili kwenye kambi hizo za Nyarugusu na Nduta mkoni Kigoma Magharibi mwa Tanzania.

Sandrine Nyaribagiza- Mkimbizi kutoka Burundi

CHIMBUKO LA MZOZO

 

Machafuko nchini Burundi yalianza April 2015 baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutaka kuwania tena  kwa mara ya tatu uongozi wa  nchi hiyo.

Ghasia zilizofuatia jaribio la mapinduzi ya kijeshi Mei 2015, zilisababisha mamia ya watu kuuawa, maelfu kupoteza makazi yao, na baadhi ya watu 420,000 kukimbilia nchi jirani.

Tangu wakati huo, Burundi imekuwa ikijaribu kutafuta suluhisho la amani la mgogoro wa kisiasa kupitia mazungumzo baina ya raia wa Burundi ambayo yanaongozwa na kanda ya Maziwa Makuu na kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa. Kwa wakati huu taifa hilo linajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa 2020.

 

MJUMBE MAALUM KWA BURUNDI

Kwa kuzingatia maazimio ya Baraza la Usalama 2248 (2015)2279 (2016) na  2303 (2016), tarehe 5 Mei 2017 Katibu Mkuu alimteua  Rais wa zamani wa Burkina Faso, Michel Kafando  kuwa mjumbe wake maalum  ili kutoa msaada katika juhudi za jumuiya ya Afrika Mashariki  (EAC) katika mazungumzo ya amani na kuratibu  juhudi za Umoja wa Mataifa  za kuendeleza mchakato wa kupata amani na maendeleo endelevu nchini Burundi.

Kikosi cha mjumbe maalum nchini Burundi kimekuwa kinashirikiana na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na Muungano wa Afrika kama sehemu ya kundi la pamoja la kiufundi (JTWG) kuunga mkono mchakato ambao hapo kabla ulikuwa unaongozwa na mshauri maalum wa katibu mkuu, Jamal Benomar.

WAKIMBIZI

 

Tangu Aprili, warundi 428,351 wamekimbilia nchi jirani kufuatia ghasia za uchaguzi mkuu. Idadi hiyo ni ile iliyoratibiwa na mpango wa kikanda kuhusu wakimbizi wa Burundi na inajumuisha wakimbizi wa Burundi tangu Aprili 2015, pamoja na  baadhi ya warundi 37,000 walioomba  hifadhi katika kanda hiyo  ya Maziwa Makuu kabla ya Aprili 2015.

Mbali na idadi hiyo ya wakimbizi , kuna warundi wengine 12,500 nchini Kenya, 4,800 Msumbiji, 3,600 Malawi, na 2,500 nchini Zambia ambao wanasaidiwa chini ya mipango ya nchi walimosaka hifadhi.

 

Wakimbizi wengine kutoka Burundi 23,000, ambao wameishi kwa miongo kadhaa nchini Tanzania hao hawapati tena msaada.

 

Ukata waleta zahma kwa wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania

Mjumbe mwingine ataeuliwa katika tume ya haki kuhusu Burundi

Taarifa Zihusianazo