DR Congo

WHO/Lindsay Mackenzie
“Bado kuna mapengo katika kukabiliana na ebola, iwe ni kijografia, kuna baadhi ya maeneo ambayo yako hatarini ambako virusi vinaweza kuwepo na tukashindwa kugundua haraka iwezekanavyo. Lakini tunahitaji kuwaza pale ambapo virusi vinakwenda, si tu kukimbizana pale inaanza kusambaa katika eneo jipya.”

Mratibu wa hatua za dharura dhidi ya Ebola nchini DRC, David Gressly

HALI HALISI

Vita, machafuko na hali mbaya ya usalama nchini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, imesababisha watu zaidi ya milioni 3 kuwa wakimbizi wa ndani na wengine zaidi ya milioni nne wamefungasha virago na kukimbilia nchi jirani za Burundi, Uganda, Tanzania, Rwanda nan chi zingine za jirani.

 

MPANGO WA UMOJA WA MATAIFA (MONUSCO)

Kazi kubwa ni kulinda raia na kudumisha Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). MONUSCO ilichukua jukumu tarehe 1 Julai 2010 kutoka kwa mpango wa awali wa opresesheni za ulinzi wa mani nchini humo (MONUC) ulioanzishwa 1999 ambao uliotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa azimio la baraza la usalama namba 1925 la tarehe 28 Mai ili kwenda sanjari na hali iliyokuwa imefikiwa wakati huo nchini DRC. Mpango mpya wa MONUSCO umeruhusiwa kutumia njia zozote zinazohitajika kutimiza jukumu lake linalohusiana pamoja na mambo mengine, kulinda raia, wahudumu wa misaada ya kibinadamu, watetezi wa haki za binadamu walio katika vitisho na kuisaidia serikali ya DRC katika juhudi zake za kurejesha Amani na utulivu. Kufikia Desemba 2017 MONUSCO ina wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa 20,688 wakijumuia walinda Amani, polisi, raia na wafanyakazi wa kujitolea. Mpango wa kwanza kabisa wa ulinzi wa amani nchini DRC ulianzishwa chini ya azimio la baraza la usalama namba 143 la tarehe 14 Julai 1960 ukijulikana kama ONUC.

HABARI ZA UN KUHUSU DRC

Bofya hapa kupata habari za Umoja wa Mataifa kuhusu DRC

HATUA ZA KIBINADAMU

Kufuatia machafuko ambayo yameathirika mamilioni ya watu nchini DRC na kuwafungisha virago mamilioni wengine, sasa mashirika la Umoja wa Mataifa na wadau wake wanafanya kila liwezekanalo kutoa msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi wa ndani na walioko nje ukiwemo wa chakula, afya, malazi, elimu na huduma zingine za msingi..

 

Taarifa Zihusianazo