Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa baraza kuu la UM kuanza ziara nchini Japan

Rais wa baraza kuu la UM kuanza ziara nchini Japan

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Joseph Deiss anatazamiwa kufanya ziara ya siku tano nchini Japan baadaye mwezi huu ambako atakuwa na fursa ya kukutana na maafisa wa ngazi za juu wa nchi za Asia.

Katika ziara yake hiyo inayoanza tarehe 26, kwanza atakutana na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Japan Naoto Kan na baadaye kuwa na mazungumzo na maafisa wengine kadhaa akiwemo waziri wa mambo ya nje Seiji Maehara.

Siku inayofuata Rais huyo anatazamiwa kuhudhuria ufunguzi wa kongamano linalowakutanisha watendaji wa ngazi ya juu kutoka kitengo cha Umoja wa Mataifa wanaoshughulilka na masuala ya Kibiologia. Ama katika ziara yake hiyo pia anatazamiwa kuwatembelea waathirika wa bomu la atomic pale atapotembelea maeneo ya Hiroshima na Nagasaki