Syria

Mtoto atibiwa baada ya mashambulio ya kemikali nchini Syria (Maktaba).
Picha: WHO_EPA/Stringer
Maadili dhidi ya matumizi ya silaha za kemikali lazima yazingatiwe. Nasihi Baraza la Usalama litekeleze wajibu wake na kusaka umoja kwenye suala hili. Baraza liongeze juhuku kukubaliana kuhusu mfumo wa uwajibishaji na niko tayari kuunga mkono juhudi hizo.

António Guterres- Katibu Mkuu wa UN, 09 APrili 2018

SYRIA

Tangu machi 2011, Syria imekuwa katika mgogoro ambao umewalazimisha watu zaidi ya 500,000 kutoroka makazi yao. Mamilioni ya raia wa Syria sio tu ni wamekimbia nchi yao, bali pia mamilioni wengine wamekuwa wakimbizi wa ndani. Mgogoro huu unachukuliwa kuwa mbaya zaidi wa kibinadamu kipindi hiki ambapo watu zaidi ya milioni 13 wanahitaji msaada na unalaumiwa kwa kusababisha wanaume, watoto pamoja na wanawake wengi wa Syria kutaabika.

 

HATUA ZA KIBINADAMU

Watu mamia kwa maelfu wameuawa na mamilioni wamelazimishwa kukimbia tangu Machi 2011, wakati mapigano yalipoanza nchini Syria kati ya serikali na makundi yanayotaka kumuondoa madarakani rais Bashar al- Assad. UN ikiwa na washirika wake inajaribu kutoa mahitaji ya msaada wa kibinadamu.

 

MJUMBE MAALUM KUHUSU SYRIA

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syrian, Staffan de Mistura, anafanya kila juhudi kuweza kuleta kwenye meza ya mazungumzo , makundi yote yanayohusika ili kuweza kumaliza vita. Mazungumzo ambayo yalipewa idhini na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 2254(2015) yanamulika utawala, ratiba na mchakato wa kupanga katiba mpya na kufanyika uchaguzi mkuu kama msingi wa mchakato wa Syria wa kumaliza mgogoro huo. Pia mazungumzo yanahusu mikakati dhidi ya ugaidi.

Taarifa Zihusianazo