Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naibu mwakilishi wa UM wa masuala ya kibinadamu azuru Haiti

Naibu mwakilishi wa UM wa masuala ya kibinadamu azuru Haiti

Naibu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu amezitembelea kambi wanamoishi waathiriwa wa tetemeko la ardhi nchini Haiti ili kutathimini shughuli za kibindamu zinazoendelea tangu kutokea kwa tetemeko hilo tarehe 12 mwezi Januari mwaka huu.

Catherine Bragg alizitembelea kambi za Mais Gate na Tabarre Issa ambapo alikutana na wahanga wa tetemeko hilo, wafanyikazi wa kutoa misaada ya kibinadaamu , polisi wa Umoja wa Mataifa UNPOL na mashirikia ya kijamii kwenye kambi.

Bibi Bragg alishughulikia suala la dhuluma za kijinsia na kusema kuwa watahakikisha kuwa wahusika wamefikishwa mbele ya sheria. Amesema kuwa watachukua hatua za kuweka vifaa zaidi vya kutoa mwangaza kwenye kambi hizo, kutoa huduma maalumu kwa waathiriwa wa dhuluma za kimapenzi na kuongeza wanajeshi ili kukomesha vitendo hivyo.

Bibi Bragg amesema kuwa UM unashirikiana na serikali na wafadhili kushughulikia masuala yakiwemo ya kubuni nafasi za ajira na ujenzi wa mashule ili kuwasaidia watu kurejea hali ya kawaida.