Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP27

Mkutano wa UN wa Mabadiliko ya Tabianchi: COP27
6 Novemba - 18 Novemba 2022: Sharm el-Sheikh, Misri
...

Ikikabiliwa na ongezeko la janga la uhaba wa nishati, halikadhalika hewa chafuzi na matukio mabaya zaidi ya hali ya hewa, COP27 inasaka kurejesha tena mshikamano kati ya mataifa na kutekeleza Mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi kwa ajili ya wakazi wa dunia na sayari dunia.

Wakuu wa nchi, serikali, mawaziri, wasuluhishi pamoja na wanaharakati wa tabianchi, mameya, wawakilishi wa mashirika ya kiraia, watendaji wa kuu wa kampuni watakutana katika mji wa pwani ya Misri, Sharm el-Sheikh katika mkutano mkubwa kuhusu tabianchi.

Mkutano huo wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, UNFCCC, COP27 utasongesha yale yaliyokubaliwa kwenye CO26 na kutoa hatua zinazoendana na kutatua dharura ya tabianchi – kuanzia kupunguza hewa chafuzi, kutekeleza ahadi za kufadhili hatua kwa tabianchi katika nchi zinazoendelea.

© UNICEF/Sebastian Rich

Tutoe mguu kwenye kichochea mwendo kasi cha uharibifu wa mazingira- Katibu Mkuu UN

Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27 ukiingia siku ya pili hii leo huko Sharm el-Sheikh nchini Misri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewakumbusha viongozi wa dunia na wote wanaohudhuria mkutano huo kwamba suluhu ya changamoto ya mabadikio ya tabianchi iko mikononi mwao na wakati wa kuchukua hatua ni sasa kwani hakuna tena muda wa kusubiri. Flora Nducha na taarifa zaidi 

Sauti
3'15"
Leah Namugerwa, mwanaharakati wa tabianchi kutoka Uganda akiwa COP27
UNIC Tokyo/Momoko Sato

COP27 ni kumbusho kwamba suluhu ya mabadiliko ya tabianchi iko mikononi mwetu:Guterres

Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27 ukiingia siku ya pili hii leo huko Sharm el-Sheikh nchini Misri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewakumbusha viongozi wa dunia na wote wanaohudhuria mkutano huo kwamba suluhu ya changamoto ya mabadikio ya tabianchi iko mikononi mwao na wakati wa kuchukua hatua ni sasa kwani hakuna tena muda wa kusubiri.

Sauti
3'15"
Simon Stiell mkuu wa UNFCCC akizungumza katika ufunguzi wa COP27
UN Japan/Momoko Sato

COP27 yafungua pazia, ni ukurasa mpya wa kufanya mambo tofauti :UNFCCC

Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP27 umefungua pazia leo huko Sharm el-Sheik, Misri, na unapaswa kuuelekeza ulimwengu kwenye utekelezaji wa mipango iliyokubaliwa hapo awali ya kukabiliana na changamoto kubwa za ubinadamu, amesema wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Simon Stiell, katibu mtendaji mpya wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Umoja wa Mataifa (UNFCCC).

Mwanamke akijarivu kuvuka maji ya mafuriko mjini Jakusko jimbo la Yobe Nigeria
© WFP/Arete/Ozavogu Abdul

Afya lazima iwe kitovu katika majadiliano ya mabadiliko ya tabianchi COP27: WHO

Katika mkesha wa mazungumzo muhimu ya mabadiliko ya tabianchi COP27, yanayoanza kesho huko Sharm-el Sheikh nchini Misri, shirika la afya la Umoja wa Mataifa Ulimwenguni WHO, limekumbusha kwamba mzozo wa mabadiliko ya tabianchi unaendelea kuwafanya watu kuwa wagonjwa na kuhatarisha maisha na kwamba afya lazima iwe msingi wa mazungumzo haya muhimu.

Mafuta kisukuku yanachangia uchafuzi wa hewa ambao unaathiri mazingira na binadamu
© Unsplash/Juniper Photon

Mabadiliko ya tabianchi yanaweza kuwa mbaya kama saratani katika baadhi ya nchi duniani: UNDP 

Bila hatua za pamoja na za haraka, mabadiliko ya tabianchi yatazidisha ukosefu wa usawa na kupanua pengo katika maendeleo ya binadamu kulingana na jukwaa jipya lililopewa jina “Human Climate Horizons” lililozinduliwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP na maabara ya athari za mabadiliko ya tabianchi.

Mandhari ya milima mjini Sharm El-Sheikh, na Qesm Sharm Ash Sheikh, Misri
Unsplash/Juanma Clemente-Alloza

COP27: Unachohitaji kufahamu kuhusu mkutano mkubwa wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa la mwaka huu.

Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi COP27 mwaka huu unafanyika huko Sharm el-Sheikh,nchini Misri wakati ambapo dunia inashuhudia ongezeko la hali mbaya ya hewa duniani kote, shida ya nishati iliyochochewa na vita vya Ukraine, na takwimu za wanasayansi zinasisitiza kwamba ulimwengu haufanyi vya kutosha kukabiliana na utoaji wa hewa ya kaboni na kulinda mustakabali wa sayari yetu.