Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP27: Unachohitaji kufahamu kuhusu mkutano mkubwa wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa la mwaka huu.

Mandhari ya milima mjini Sharm El-Sheikh, na Qesm Sharm Ash Sheikh, Misri
Unsplash/Juanma Clemente-Alloza
Mandhari ya milima mjini Sharm El-Sheikh, na Qesm Sharm Ash Sheikh, Misri

COP27: Unachohitaji kufahamu kuhusu mkutano mkubwa wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa la mwaka huu.

Tabianchi na mazingira

Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi COP27 mwaka huu unafanyika huko Sharm el-Sheikh,nchini Misri wakati ambapo dunia inashuhudia ongezeko la hali mbaya ya hewa duniani kote, shida ya nishati iliyochochewa na vita vya Ukraine, na takwimu za wanasayansi zinasisitiza kwamba ulimwengu haufanyi vya kutosha kukabiliana na utoaji wa hewa ya kaboni na kulinda mustakabali wa sayari yetu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema COP27 lazima itoe "malipo ya awali" kwenye kusaka majawabu ya changamoto za mabadiliko ya tabianchi na lazima yalingane na viwango vya ukubwa wa tatizo, je viongozi watatoa?”

Idhaa ya Umoja wa Mataifa itakuwepo katika mkutano huo na kukufahamisha katika kipindi chote cha  wiki mbili za mkutano huo unaoanza rasmi tarehe 6 Novemba, lakini kabla ya timu yetu ya vyombo vya habari vya habari kuelekea ufukweni mwa Bahari Nyekundu, tumekusanya mwongozo huu kwa baadhi ya mambo muhimu zaidi unayohitaji kujua.

wajumbe wakiwa wamekaa katika ukumbi kuu wa mkutano wa COP26 huko Glasgow, Scotland
UNFCCC/Kiara Worth
wajumbe wakiwa wamekaa katika ukumbi kuu wa mkutano wa COP26 huko Glasgow, Scotland

Historia ya COPs

Mikutano wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa tabianchi au kwa kifupi COPs ndio mikutano mikubwa na muhimu zaidi ya kila mwaka inayohusiana na tabianchi kwenye sayari.

Mwaka 1992, Umoja wa Mataifa iliandaa Mkutano wa Dunia huko Rio de Janeiro, Brazil, ambapo Mkataba wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC ulipitishwa na wakala wake wa kuratibu kile tunacholikana sasa kama sekretarieti ya Umoja wa Mataifa ya Mabadiliko ya Tabianchi - iliwekwa.

Katika mkataba huu, mataifa yalikubaliana “kuimarisha viwango vya gesi chafuzi katika anga ili kuzuia muingiliano hatari kutokana na shughuli za binadamu kwenye mifumo wa hali ya hewa.” Hadi sasa, nchi 197 zimetia saini mkataba huu.

Tangu mwaka 1994, wakati mkataba huo ulipoanza kutekelezwa, kila mwaka Umoja wa Mataifa umekuwa ukiwaleta pamoja karibu kila nchi zote duniani kwa ajili ya mikutano ya kimataifa ya tabianchi au “COPs”, ambayo ni kifupi cha “Mkutano wa nchi wanachama”.

Wakati wa mikutano hii, mataifa yamejadili upanuzi mbalimbali wa mkataba wa awali ili kuweka vikwazo vya kisheria juu ya utoaji wa hewa chafu, kwa mfano, Itifaki ya Kyoto mwaka 1997 na Mkataba wa Paris uliopitishwa mwaka 2015, ambapo nchi zote za dunia zilikubali kuongeza juhudi katika kujaribu na kupunguza ongezeko la joto duniani hadi nyuzi joto 1.5 na kuongeza ufadhili kwenye mapambano ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mwaka huu ni mkutano wa 27 wa kilele wa kila mwaka, au COP27.

Mashirika ya kiraia wakiandamana kwenye mkutano wa COP26  Glasgow, Scotland.
UN News/Laura Quinones
Mashirika ya kiraia wakiandamana kwenye mkutano wa COP26 Glasgow, Scotland.

Tofauti kati ya COP27 na COP nyingine ni ipi?

COP26 ya mwaka jana (2021), ambayo iliadhimisha miaka mitano tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Paris (mwaka mmoja ulirukwa kwa sababu ya janga la COVID19), ilifikia kilele cha Mkataba wa Hali ya Hewa wa Glasgow, ambao uliweka lengo la kupunguza ongezeko la joto duniani hadi nyuzi joto 1.5, lakini " na mapigo ya moyo dhaifu”, kama Rais wa Uingereza wa wakati huo ulivyotangaza.

Maendeleo yalifanywa ili kufanya Mkataba wa Paris ufanye kazi kikamilifu, kwa kukamilisha maelezo ya utekelezaji wake wa vitendo, unaojulikana pia kama Kitabu cha Sheria cha Paris.

Katika COP26 nchi zilikubali kutoa ahadi zenye nguvu zaidi mwaka huu, ikijumuisha mipango iliyowekwa kitaifa yenye malengo makubwa zaidi. Hata hivyo, ni nchi 23 tu kati ya 193 ambazo zimewasilisha mipango yao kwa Umoja wa Mataifa hadi sasa.

Glasgow pia iliona ahadi nyingi zilizotolewa ndani na nje ya vyumba vya mazungumzo kuhusu ahadi za sifuri, ulinzi wa misitu na ufadhili wa tabianchi, miongoni mwa masuala mengine mengi.

Kulingana na taarifa ya dira ya Rais, COP27 itahusu kuhama kutoka kwenye mazungumzo, na "kupanga utekelezaji" kwa ahadi zote hizi na ahadi zilizotolewa.

Misri imetoa wito wa kuchukua hatua kamili, kwa wakati muafaka, jumuishi na kwa viwango cha kuzingatia hali za mashinani.

Kulingana na wataalamu, kando na kukagua jinsi ya kutekeleza Kitabu cha Sheria cha Paris, mkutano huo pia utafanya mazungumzo kuhusu baadhi ya mambo ambayo yalisalia bila kujumuisha baada ya Glasgow.

Masuala haya ni pamoja na ufadhili wa "hasara na uharibifu" ili nchi zilizo mstari wa mbele wa mgogoro huo ziweze kukabiliana na matokeo ya mabadiliko ya tabianchi ambayo yanaenda zaidi ya kile wanaweza kukabiliana nacho, na utimilifu wa ahadi ya dola bilioni 100 kila mwaka kutokana na fedha za kukabiliana na hali hiyo, kutoka mataifa yaliyoendelea hadi nchi za kipato cha chini.

Mazungumzo hayo pia yatajumuisha mijadala ya kiufundi, kwa mfano, kubainisha njia ambayo mataifa yanapaswa kupima uzalishaji wao kivitendo ili kuwe na uwanja sawa kwa kila mtu.

Majadiliano haya yote yatafungua njia kwa Uchukuaji Hisa wa Kwanza wa Kimataifa katika COP28, ambao katika mkutano wa 2023 utatathmini maendeleo ya pamoja ya kimataifa kuhusu upunguzaji, urekebishaji, na njia za utekelezaji wa Makubaliano ya Paris.

Dunia ni lazima iongeze haraka hatua na matamanio ya kupunguza asilimia nyingine 25 ya hewa chafuzi ifikapo 2030
Picha:UNEP
Dunia ni lazima iongeze haraka hatua na matamanio ya kupunguza asilimia nyingine 25 ya hewa chafuzi ifikapo 2030

Malengo makubwa ya mwaka huu ni yapi?

 

1. Kupunguza: jinsi gani nchi zinapunguza uzalishaji wao ?

Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi inarejelea juhudi za kupunguza au kuzuia utoaji wa gesi chafuzi. Kupunguza kunaweza kumaanisha kutumia teknolojia mpya na vyanzo vya nishati mbadala, kufanya vifaa vya zamani kuwa na ufanisi zaidi wa nishati, au kubadilisha mazoea ya usimamizi au tabia ya watumiaji.

Nchi zinatarajiwa kuonyesha jinsi zinapanga kutekeleza wito wa mkataba wa Glasgow, kukagua mipango yao ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuunda programu ya kazi inayohusiana na kukabiliana na hali hiyo.

 

Hii ina maana kuwa zitawasilisha shabaha kubwa zaidi za kufikia lengo la kupunguza hewa chafu ifikapo mwaka 2030, kwani malengo ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi ya Umoja wa Mataifa yamesema kuwa mipango ya sasa bado haitoshi kuepusha janga la ongezeko la joto.

Wakulima wa kaskazini mwa Haiti wanashughulikia hatua ambazo zitazuia mmomonyoko wa mashamba yao.
© WFP Haiti/Theresa Piorr
Wakulima wa kaskazini mwa Haiti wanashughulikia hatua ambazo zitazuia mmomonyoko wa mashamba yao.

2. Marekebisho: ni jinsi gani nchi zitabadilika na kusaidia nchi zingine kufanya vivyo hivyo?

Mabadiliko ya tabianchi yapo. Zaidi ya kufanya kila tuwezalo kupunguza utoaji wa hewa chafuzi na kupunguza kasi ya ongezeko la joto duniani, nchi lazima pia zikabiliane na athari za mabadiliko ya tabianchi ili ziweze kuwalinda raia wao.

Kuanguka hutofautiana kulingana na eneo. Inaweza kumaanisha hatari ya moto zaidi au mafuriko, ukame, siku za joto au baridi au kupanda kwa kina cha bahari.

Katika COP26, wajumbe walipitisha programu ya kazi kuhusu lengo la kimataifa la kukabiliana na hali iliyoanzishwa katika Mkataba wa Paris.

Mpango huo uliwekwa ili kuzipa jamii na nchi ujuzi na zana ili kuhakikisha kwamba hatua za kukabiliana na hali wanazochukua, kwa hakika zinaupeleka ulimwengu kuelekea mustakabali unaostahimili hali ya hewa.

Urais wa COP27 unatarajia mataifa kukamata na kutathmini maendeleo yao kuelekea kuimarisha uthabiti na kusaidia jamii zilizo hatarini zaidi. Hii ina maana kwamba nchi zinatoa ahadi za kina zaidi na kabambe katika vipengele vya kukabiliana na mipango yao ya kitaifa ya hali ya hewa.

Mwaka jana, nchi zilizoendelea zilikubali angalau kufadhili mara mbili kwa ajili ya kukabiliana na hali hiyo, na wadau wengi wanatoa wito wa kuwepo kwa viwango vikubwa zaidi vya ufadhili wa kukabiliana na hali hiyo ili kuendana na kiasi ambacho sasa kinatumika kupunguza, kama ilivyoanzishwa katika Mkataba wa Paris.

Hakika hii itakuwa mada kubwa ya mazungumzo huko Sharm el-Sheikh.

UNFCCC ni wazi kwamba ili kukabiliana na hatari za sasa na zijazo za mabadiliko ya tabianchi ni muhimu kuongeza kwa kiasi kikubwa kiwango cha fedha za kukabiliana na hali hiyo, kutoka kwa vyanzo vyote - vyanzo vya umma na vya kibinafsi. Wachezaji wote lazima wajitokeze - serikali, taasisi za fedha, na sekta ya kibinafsi.

Dola za kimarekani
Picha ya UN
Dola za kimarekani

3. Fedha za Tabianchi: Tembo ambaye hatoki nje ya chumba cha mazungumzo

Ufadhili wa tabianchi utakuwa mada kuu kwa mara nyingine tena katika COP27, mijadala mingi inayohusiana na fedha tayari iko kwenye ajenda, huku nchi zinazoendelea zikitoa wito mkubwa kwa nchi zilizoendelea kuwahakikishia msaada wa kutosha na wa kutoa kifedha, haswa kwa walio hatarini zaidi.

Pengine tutasikia mengi kuhusu ahadi ya kila mwaka ya dola bilioni 100 na mataifa yaliyoendelea ambayo hayatekelezwi. Mnamo mwaka wa 2009 huko Copenhagen, nchi tajiri zilijitolea kutoa ufadhili huu, lakini ripoti rasmi bado zinaonesha kuwa lengo hili linakosekana. Wataalam wanatarajia COP27 kufanya ahadi hii kuwa ukweli mnamo 2023.

Urais wa Misri unalenga kufuatilia hili na ahadi nyingine na ahadi zilizotolewa katika COP zilizopita.

Tarene 3 Septemba Rahim mwenye umri wa miaka 4 akiwa amesimama kwenye kifusi cha nyumba yao iliyosambaratishwa na mafuriko nchini Pakistan
© UNICEF/Asad Zaidi
Tarene 3 Septemba Rahim mwenye umri wa miaka 4 akiwa amesimama kwenye kifusi cha nyumba yao iliyosambaratishwa na mafuriko nchini Pakistan

Je, suala la ‘Hasara na Uharibifu’ tunalolisikia sana ni nini?

Mabadiliko ya tabianchi, kupitia matukio mabaya ya hali ya hewa kama vile vimbunga vya kitropiki, hali ya jangwa na kupanda kwa kina cha bahari, husababisha uharibifu mkubwa kwa nchi.

Kwa sababu kukithiri kwa haya "majanga ya asili" kunasababishwa na kuongezeka kwa uzalishaji wa gesi chafuzi, hasa kutoka nchi tajiri zilizoendelea kiviwanda, nchi zinazoendelea ambazo mara nyingi zimeathirika zaidi zinahoji kwamba zinapaswa kupokea fidia.

Denmark iligonga vichwa vya habari wakati wa wiki za hivi karibuni katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa baada ya kuwa nchi ya kwanza kutangaza kwamba itatoa dola milioni 13 kwa nchi zinazoendelea ambazo zimekumbwa na uharibifu kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Suala la malipo haya, linalojulikana kama "hasara na uharibifu" litakuwa mada kubwa zaidi ya mjadala katika COP27, hata wakati bado halijawekwa rasmi kwenye ajenda.

Kundi la 77 na China (ambalo kimsingi linajumuisha mataifa yote yanayoendelea) limeomba kuiongeza kwenye ajenda, ambayo itahitaji maafikiano katika nchi zote katika siku ya kwanza ya mazungumzo.

Hadi sasa, kumekuwa na majadiliano kuhusu kuanzisha mfuko wa Hasara na Uharibifu, lakini hakuna kitu halisi. Wataalamu kama vile Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Kibinadamu na Tabianchi, Ian Fry, wanatumai kuongeza kasi zaidi na "kuikamilisha".

“Kuna nchi kubwa zilizoendelea ambazo zina wasiwasi juu yake na kuangalia suala hili kwa mtazamo wa kila mchafuzi wa mazingira analipa. Sasa, nchi zilizoathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi na kuteseka kwa gharama zinalazimika kushughulikia gharama hizo zenyewe.” Alisema Fry na kuogeza kuwa

“Kwa hivyo, ni wakati wa nchi kubwa, wazalishaji wakuu, kusimama na kusema, 'lazima tufanye kitu, lazima tutoe mchango kwa nchi hizi zilizo hatarini'", aliambia Idhaa ya Umoja wa Mataifa wakati wa mahojiano ya hivi karibuni.

Fundi akirekebisha mambo kwenye mtambo wa sola nchini Thailand
© ADB
Fundi akirekebisha mambo kwenye mtambo wa sola nchini Thailand

Je, vita vya Ukraine vinaathiri vipi haya yote?

Kulingana na Ilana Seid, Mwakilishi wa Kudumu wa Palau katika Umoja wa Mataifa, na mpatanishi wa tabianchi, COP hii itakuwa "ya kutatanisha" kutokana na mazingira ya sasa ya kijamii na kisiasa na mgogoro wa nishati.

"Vita vya Ukraine vilitokea, kwa hivyo kuna mambo mengi ambayo nchi nyingi zilikubali, na sasa haziwezi kufanya. Kutokana na vita, mazingira yamebadilika,” alieleza.

Kwa hakika, uvamizi wa Urusi kwa Ukraine umesababisha mfumuko wa bei duniani, nishati, chakula na mgogoro kwenye ugavi. Nchi kama vile Ujerumani zimelazimika kurudisha nyuma kwa muda mfupi malengo yao ya tabianchi, wakati Kikundi cha Kikaokazi cha Tabianchi cha China na Marekani kilichotangazwa huko Glasgow sasa kimesimamishwa.

COP27 ina uwezekano mkubwa wa kuona kurudi nyuma katika ahadi ambazo nchi zingine zilifanya mwaka jana.

Hata hivy Mwandishi Maalum Ian Fry anaona kwamba vita hivyo vinaweza pia kuwa "wito wa kuwaamsha" mataifa kujitegemea kwa nishati.

Anasema kuwa njia ya bei nafuu zaidi ya kufanya hivyo ni kupitia upya, ambayo ni muhimu katika kupunguza uzalishaji.

"Tunaiona Ureno ikielekea kwenye nishati jadidifu kwa asilimia 100, tunajua Denmark pia inafanya hivyo, na nadhani hiyo itazisukuma nchi nyingine kuona hitaji la kuwa na mbadala na kujitosheleza kwa nishati", aliiambia Idhaa ya Umoja wa Mataifa.

Wanaharakati vijana wa mazingira wakiwa kwenye maandamano huko Glasgow, Scotland Ijumaa 05 Novemba 2021 wakati wa COP26
UN News/Laura Quinones
Wanaharakati vijana wa mazingira wakiwa kwenye maandamano huko Glasgow, Scotland Ijumaa 05 Novemba 2021 wakati wa COP26

Je, asasi za kiraia zitashiriki katika COP, au wajumbe wanaowakilisha mataifa yao wenyewe?

Hafla kuu itafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Sharm el-Sheikh, kuanzia tarehe 6-18 Novemba, 2022.

Hadi kufikia sasa, kuna zaidi ya watu 30,000 waliojiandikisha kuhudhuria kuwakilisha serikali, wafanyabiashara, NGOs, na mashirika ya kiraia.

Nchi 197 wanachama wa Mkataba wa UNFCCC, mara nyingi hukutana kwa vikundi au "kambi", kujadili pamoja kama vile G77 na Uchina, Kundi la Afrika, Nchi zinazoendelea zenye uchumi mdogo, Majukwaa chini ya miavuli mbalimbali, Nchi za Visiwa Vidogo Zinazoendelea, na Muungano Huru wa Amerika ya Kusini na Karibiani.

Mazungumzo hayo pia yanajumuisha waangalizi, ambao hawana sehemu rasmi ndani yao lakini wanaingilia kati na kusaidia kudumisha uwazi. Waangalizi ni pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa, mashirika ya kiserikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, vikundi vya kidini, na waandishi wa habari.

Lakini kando na mazungumzo rasmi, kutakuwa na vyumba vya mikutano, sehemu ya mabanda, na maelfu ya matukio yanayotokea, yakigawanywa kwa siku za mada.

Mada za mwaka huu ni: Fedha, Sayansi, Vijana na Vizazi Vijavyo, Utoaji kaboni, Urekebishaji na Kilimo, Jinsia, Maji, Jumuiya ya Kiraia, Nishati, Bioanuwai na Suluhisho (Dhima mpya zaidi ya COP hii).

Kama kawaida, mkutano utafanyika katika kanda mbili - Eneo la Bluu na Eneo la Kijani, ambazo mwaka huu ziko karibu.

Eneo la Bluu ni nafasi inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa ambapo mazungumzo yanaandaliwa na, ili kuingia, wahudhuriaji wote lazima wapewe vibali na Sekretarieti ya UNFCCC.

Mwaka huu kutakuwa na mabanda 156 ndani ya Eneo la Bluu, hii ni mara mbili ya kiasi ikilinganisha na mkutano wa mwaka jana huko Glasgow. Mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa, nchi na kanda zitawakilishwa, na pia kutakuwa na kwa mara ya kwanza banda la Vijana na kilimo cha mazao ya chakula.

Eneo la Kijani linasimamiwa na Serikali ya Misri na liko wazi kwa umma uliosajiliwa. Itajumuisha matukio, maonesho, warsha na mazungumzo ya kukuza mazungumzo, uhamasishaji, elimu, na kujitolea juu ya hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kulingana na Ofisi ya Rais, Eneo la Kijani litakuwa jukwaa ambapo jumuiya ya wafanyabiashara, vijana, jumuiya za kiraia na za kiasili, wasomi, wasanii na jumuiya za wanamitindo kutoka kote ulimwenguni wanaweza kujieleza na sauti zao kusikika.

Mwaka huu, Eneo la Kijani pia litajumuisha "eneo la maandamano" maalum, na chumba kikubwa cha kupumzika cha nje na nafasi ya uwani.

Wapatanishi wakiashiria kufungwa kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, COP26, uliofunguliwa huko Glasgow, Scotland, tarehe 31 Oktoba. Mkutano huo ulitafuta ahadi mpya za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
UN News/Laura Quinones
Wapatanishi wakiashiria kufungwa kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, COP26, uliofunguliwa huko Glasgow, Scotland, tarehe 31 Oktoba. Mkutano huo ulitafuta ahadi mpya za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Je, ninawezaje kufuata mijadala na matukio nikiwa nyumbani?

  • Kufuatia ukurasa wetu maalum wa COP27

Link : https://news.un.org/en/events/cop27

 

  • Kujiandikisha sasa kwa jarida letu la kila siku la hali ya hewa COP27

Link : https://news.un.org/en/newsletter/climate-change

 

  • Kujiandikisha kwa kusikiliza podcast  toleo maalum la COP27

Link : https://news.un.org/en/audio-product/podcast-the-lid-is-on

  • Kufuatia Habari za UN kwenye Twitter @HabarizaUN
  • Kujiandikisha kwa Chaneli rasmi ya Youtube ya COP27

Link: https://www.youtube.com/channel/UC7R00Uc-iMohAj3_ljLuGMQ