Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP27

Mkutano wa UN wa Mabadiliko ya Tabianchi: COP27
6 Novemba - 18 Novemba 2022: Sharm el-Sheikh, Misri
...

Ikikabiliwa na ongezeko la janga la uhaba wa nishati, halikadhalika hewa chafuzi na matukio mabaya zaidi ya hali ya hewa, COP27 inasaka kurejesha tena mshikamano kati ya mataifa na kutekeleza Mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi kwa ajili ya wakazi wa dunia na sayari dunia.

Wakuu wa nchi, serikali, mawaziri, wasuluhishi pamoja na wanaharakati wa tabianchi, mameya, wawakilishi wa mashirika ya kiraia, watendaji wa kuu wa kampuni watakutana katika mji wa pwani ya Misri, Sharm el-Sheikh katika mkutano mkubwa kuhusu tabianchi.

Mkutano huo wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, UNFCCC, COP27 utasongesha yale yaliyokubaliwa kwenye CO26 na kutoa hatua zinazoendana na kutatua dharura ya tabianchi – kuanzia kupunguza hewa chafuzi, kutekeleza ahadi za kufadhili hatua kwa tabianchi katika nchi zinazoendelea.

Mtoto mwenye umri wa miaka 11 akijipatia ahueni ya joto kali kwa kucheza kwenye chemchem ya maji huko  Uzbekhstan
UNICEF/Pirozzi

Watoto milioni 559 duniani kote wanataabika na joto kali kwa sasa, idadi itaongeza na kufikia zaidi ya bilioni 2 mwaka 2050.

Kuelekea mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP27utakaofanyika nchini Misri barani Afrika, shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto UNICEF wametoa ripoti ya kuonesha athari za mabadiliko ya tabianchi kwa watoto katika kipindi cha kuanzia sasa mpaka mwaka 2050.