Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

07 NOVEMBA 2022

07 NOVEMBA 2022

Pakua

Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Assumpta Massoi akimulika tabianchi na mazingira kwa kiasi kikubwa kutokana na mkutano wa mabadiliko ya tabianchi  unaofanyika Misri.

  1. Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27 ukiingia siku ya pili hii leo huko Sharm el-Sheikh nchini Misri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewakumbusha viongozi wa dunia na wote wanaohudhuria mkutano huo kwamba suluhu ya changamoto ya mabadikio ya tabianchi iko mikononi mwao na wakati wa kuchukua hatua ni sasa kwani hakuna tena muda wa kusubiri.
  2. Nchini Gabon,  Benki ya Dunia imerejesha matumaini kwa jamii za wavuvi ambao uvuvi ndio tegemeo kuu la kujipatia kipato wakati huu ambapo uvuvi haramu ulianza kuleta shaka, shuku na hofu miongoni mwa jamii lakini sasa hatua za pamoja za uvuvi unaojali mazingira umeleta amani.
  3. Makala: tunaelekea nchini Colombia ambako kikundi kinachoongozwa na wanawake wanasayansi cha Blue Indigo kinasaidia katika urejeshaji wa miamba ya matumbawe ili kuokoa mifumo ya ikolojia baharini iliyoharibiwa na mabadiliko ya tabianchi pamoja na shughuli za utalii.
  4. Mashinani: Jyotsna Puri, Makamu Rais wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD akiongoza Idara ya Mkakati na Ufahamu na anatoa wito wa usaidizi kwa wakulima wadogo ambao ndio huathiriwa zaidi na madhara ya mabadiliko ya tabianchi.
Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
13'2"