Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanasayansi wanawake huko Colombia watumia taaluma yao kurejesha matumbawe yaliyoharibiwa kutokana na shughuli za kibinadamu

Wanasayansi wanawake huko Colombia watumia taaluma yao kurejesha matumbawe yaliyoharibiwa kutokana na shughuli za kibinadamu

Pakua

Shughuli za utalii, uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi zimechochea kuleta wasiwasi kwa wananchi wa kisiwa cha San Andres nchini Colombia kutokana na matumbawe waliyokuwa wanategemea kuvutia watalii kuanza kuharibika na samaki wa asili nao wameanza kupotea.

Shirika la Blue Indigo linaloongozwa na wanawake wanasayansi wa kisiwani humo limedhamiria kutumia taaluma yao kuwaleta pamoja wanajamii katika kuhakikisha wanarejesha mifumo asilia ya miamba ya matumbawe huku wakiendeleza utalii endelevu na wananchi kuendelea na uvuvi ili kujipatia kipato. Tuungane na Leah Mushi katika Makala hii.

Audio Credit
Flora Nducha/Leah Mushi
Sauti
4'52"
Photo Credit
Blue Indigo