Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP27

Mkutano wa UN wa Mabadiliko ya Tabianchi: COP27
6 Novemba - 18 Novemba 2022: Sharm el-Sheikh, Misri
...

Ikikabiliwa na ongezeko la janga la uhaba wa nishati, halikadhalika hewa chafuzi na matukio mabaya zaidi ya hali ya hewa, COP27 inasaka kurejesha tena mshikamano kati ya mataifa na kutekeleza Mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi kwa ajili ya wakazi wa dunia na sayari dunia.

Wakuu wa nchi, serikali, mawaziri, wasuluhishi pamoja na wanaharakati wa tabianchi, mameya, wawakilishi wa mashirika ya kiraia, watendaji wa kuu wa kampuni watakutana katika mji wa pwani ya Misri, Sharm el-Sheikh katika mkutano mkubwa kuhusu tabianchi.

Mkutano huo wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, UNFCCC, COP27 utasongesha yale yaliyokubaliwa kwenye CO26 na kutoa hatua zinazoendana na kutatua dharura ya tabianchi – kuanzia kupunguza hewa chafuzi, kutekeleza ahadi za kufadhili hatua kwa tabianchi katika nchi zinazoendelea.

Mitambo ya sola katika ofisi za UNDP jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kama sehemu ya kuongoza kwa vitendo katika hatua za kulinda mazingira.
Sawiche Wamunza/UNDP Tanzania

Tanzania kushirikiana na SADC kuzalisha nishati jadidifu

Wakati wiki ya kwanza ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP27 unaondelea huko Sharm el-Sheikh nchini Misri ikiwa inaelekea ukingoni na masuala mbalimbali yakiwa yamejadiliwa ikiwemo ufadhili wa miradi ya tabianchi, malipo ya fidia kwa nchi maskini kutokana na hasara na uharibifu uliosababishwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, Tanzania imeitisha mkutano na nchi wanachama Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC ili kuhimiza ushirikiano katika kuzalisha nishati jadidifu.

10 NOVEMBA 2022

Katika Jarida la habari la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea 

-Huko Sharm el Sheikh kwenye mkutno wa COP27 vijana watoa wito kwa nchi wachafuzi wa mazingira kugharamia hasara na uharibifu wa janga hilo

-Nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO washikana na jeshi la serikali FARDC kuendesha doria kulinda raia

-Nchini Lebanon shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na wadau wa chanjo wafikisha chanjo 600,000 kwa ajili ya kampeni dhidi ya kipindupindu itakayoanza Jumamosi

Sauti
13'40"