Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP27

Mkutano wa UN wa Mabadiliko ya Tabianchi: COP27
6 Novemba - 18 Novemba 2022: Sharm el-Sheikh, Misri
...

Ikikabiliwa na ongezeko la janga la uhaba wa nishati, halikadhalika hewa chafuzi na matukio mabaya zaidi ya hali ya hewa, COP27 inasaka kurejesha tena mshikamano kati ya mataifa na kutekeleza Mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi kwa ajili ya wakazi wa dunia na sayari dunia.

Wakuu wa nchi, serikali, mawaziri, wasuluhishi pamoja na wanaharakati wa tabianchi, mameya, wawakilishi wa mashirika ya kiraia, watendaji wa kuu wa kampuni watakutana katika mji wa pwani ya Misri, Sharm el-Sheikh katika mkutano mkubwa kuhusu tabianchi.

Mkutano huo wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, UNFCCC, COP27 utasongesha yale yaliyokubaliwa kwenye CO26 na kutoa hatua zinazoendana na kutatua dharura ya tabianchi – kuanzia kupunguza hewa chafuzi, kutekeleza ahadi za kufadhili hatua kwa tabianchi katika nchi zinazoendelea.

Mandhari ya milima mjini Sharm El-Sheikh, na Qesm Sharm Ash Sheikh, Misri
Unsplash/Juanma Clemente-Alloza

COP27: Unachohitaji kufahamu kuhusu mkutano mkubwa wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa la mwaka huu.

Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi COP27 mwaka huu unafanyika huko Sharm el-Sheikh,nchini Misri wakati ambapo dunia inashuhudia ongezeko la hali mbaya ya hewa duniani kote, shida ya nishati iliyochochewa na vita vya Ukraine, na takwimu za wanasayansi zinasisitiza kwamba ulimwengu haufanyi vya kutosha kukabiliana na utoaji wa hewa ya kaboni na kulinda mustakabali wa sayari yetu.