Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya tabianchi yanaweza kuwa mbaya kama saratani katika baadhi ya nchi duniani: UNDP 

Mafuta kisukuku yanachangia uchafuzi wa hewa ambao unaathiri mazingira na binadamu
© Unsplash/Juniper Photon
Mafuta kisukuku yanachangia uchafuzi wa hewa ambao unaathiri mazingira na binadamu

Mabadiliko ya tabianchi yanaweza kuwa mbaya kama saratani katika baadhi ya nchi duniani: UNDP 

Tabianchi na mazingira

Bila hatua za pamoja na za haraka, mabadiliko ya tabianchi yatazidisha ukosefu wa usawa na kupanua pengo katika maendeleo ya binadamu kulingana na jukwaa jipya lililopewa jina “Human Climate Horizons” lililozinduliwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP na maabara ya athari za mabadiliko ya tabianchi.

Jukwaa hilo limeundwa ili kuwawezesha watu na watoa maamuzi kila mahali, duniani kuonyesha nini mabadiliko ya tabianchi yanaweza kumaanisha kwa maisha ya watu kupitia mabadiliko ya vifo, uwezo wa kupata riziki na matumizi ya nishati. 

Kwa mfano UNDP inasema, huko Dhaka, mji mkuu wa Bangladesh, kutokana na hali ya utoaji kiasi kikubwa cha hewa chafuzi vifo vya ziada hadi kufikia 2100 vya kutokana na mabadiliko ya tabianchi saw ana watu 132 katika kila watu 100,000 kwa mwaka vitatokea na itakuwa karibu mara mbili ya kiwango cha sasa cha vifo vya kila mwaka vya Bangladesh vinavyotokana na saratani zote, na mara 10 ya vifo vyake vya kila mwaka vya ajali za barabarani. 

Nyadend Majok akiwa amesismama kando ya shamba lake la mtama lililosambaratishwa na mafuriko nchini Sudan Kusini
© WFP/Gabriela Vivacqua
Nyadend Majok akiwa amesismama kando ya shamba lake la mtama lililosambaratishwa na mafuriko nchini Sudan Kusini

Kuna pengo kubwa miongoni mwa nchi 

Kwa mujibu wa jukwaa hili ulinganisho wa athari za kiafya za mabadiliko ya tabianchi katika nchi zote unaashiria mustakabali unaoongeza pengo la usawa kati ya nchi za G20 ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa hewa ukaa CO2 ambapo theluthi moja miongoni mwao itapata viwango vya ziada vya vifo kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi.  

Jukwaa hilo limeongeza kuwa lakini hali hii inaongezeka hadi karibu robo tatu kwa nchi zinazoendfelea na kuongeza kwa kiasi kikubwa pengo la usawa katika miongo ijayo. 

Kwa mujibu wa mkuu wa UNDP Achim Steiner "Mwaka 2022, jamii katika kila kona ya dunia zinashuhudia dharura ya mabadiliko ya tabianchi ambayo inapiga kwa kasi na kwa nguvu zaidi kuliko ilivyotarajiwa katika sehemu nyingi, ikiwakilisha tishio kwa maisha yetu ya baadaye na hatari ya kweli ambayo lazima ishughulikiwe hapa na sasa. Kwa kuzingatia athari za mabadiliko ya hali yatabianchi katika masuala kama vile vifo, kazi na matumizi ya nishati, jukwaa la New Horizons for human climate linaweka takwimu muhimu na uchambuzi mikononi mwa watunga sera, kusaidia nchi kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi inapohitajika zaidi. Kwa mfano, jukwaa linaonyesha kuwa juhudi kubwa za kimataifa kuelekea malengo ya mkataba wa Paris zinaweza kupunguza makadirio ya vifo kutokana na joto kali katika mwaka wa 2100 kwa zaidi ya asilimia 80%, na hivyo kuokoa makumi ya mamilioni ya Maisha ya watu.” 

Kila jamii inashuhudia mabadiliko ya tabianchi 2022 

UNDP imesema kwa mwaka huu wa 2022 kila jamii inashuhudia mabadiliko ya tabianchi huku takwimu mpya zinaonyesha kuwa mabadiliko ya tabianchi yataongeza pengo la usawa ndani ya nchi.  

Mafuta kisukuku yanachangia uchafuzi wa hewa ambao unaathiri mazingira na binadamu
© Unsplash/Juniper Photon
Mafuta kisukuku yanachangia uchafuzi wa hewa ambao unaathiri mazingira na binadamu

Kwa mfano Barranquilla, jiji la bandari kaskazini mwa Colombia, kutokana na utoaji sana wa hewa chafuzi kiwango cha ziada cha vifo 2100 kwa sababu ya joto cha joto kali sawa na watu 37 katika kila watu 100,000 kwa mwaka hii ni mara tano zaidi ya kiwango cha vifo vya Colombia vinavyotokana na saratani ya matiti kila mwaka.  

Hali hii inaongeza idadi ya viwango vya vifo kutokana na mabadiliko ya tabianchi ikilinganishwa na mji mkuu wa Bogotá. 

Naye Sol Hsiang kutoka Impact Lab ambaye ni profesa wa masuala ya suera za umma na mkuu wa chou kikuu cha Berkeley California amesema “Maabara ya athari za mabadiliko ya tabianchi huchanganya huchanganya takwimu za kimataifa, uchanganuzi mkubwa wa takwimu, na mifano ya kina ya mabadiliko ya tabianchi ili kukadiria gharama za changamoto hiyo na manufaa ya kupunguza hewa chafuzi. Kwa kuzingatia utafiti thabiti, inaonyesha jinsi athari za siku za usoni za mabadiliko ya tabianchi zinavyoangukia kwa kiasi kikubwa katika maeneo ambayo yana joto zaidi na mara nyingi maskini zaidi, na kuzidisha pengo lililopo la usawa. Kwa bahati nzuri, ulimwengu bado unaweza kubadilisha mkondo kwa kupunguza kwa kiasi kikubwa hewa chafuzi."  

Takwimu mpya zinaonyesha haja ya kuchukua hatua haraka, sio tu kupunguza mabadiliko ya tabianchi lakini pia kukabiliana na matokeo yake.  

Kwa mfano, huko Faisalabad, Pakistani, hata kwa kupunguza kwa wastani, vifo vya ziada kutokana na mabadiliko ya tabianchi na kufikia wastani wa watu 36 kwa kila watu 100,000 kila mwaka kati ya 2020-2039.  

Bila kupanua kwa kiasi kikubwa juhudi za kukabiliana na hali hiyo, Faisalabad inaweza kutarajia viwango vya vifo vinavyohusiana na mabadiliko ya tabianchi kila mwaka kufikia karibu mara mbili, idadi ambayo ni vifo 67 kwa kila vifo 100,000 ifikapo katikati ya karne hii.  

Na hilo ni ongezeko linalokaribia kuua kama vile kiharusi, kwa sasa ugonjwa ambao ni moja ya sababu kuu tatu za vifo nchini Pakistan.