Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tubadili mitindo ya maisha na kuishi kwa kujali utunzaji wa mazingira : Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza wakat iwa uzinduzi wa mpango wa mtindo wa maisha huko Narmada nchiini India.
UN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza wakat iwa uzinduzi wa mpango wa mtindo wa maisha huko Narmada nchiini India.

Tubadili mitindo ya maisha na kuishi kwa kujali utunzaji wa mazingira : Guterres

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko ziarani nchini India, amezindua mpango wa Mitindo wa Maisha unaojali utunzaji wa Mazingira na kuhimiza wananchi wote kubadili mitindo yao ya maisha na Kuishi maisha ambayo yanazingatia si tu kulinda mazingira bali pia kujali kizazi cha sasa na cha baadae.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika Sanamu ya Umoja lilikoko eneo la Ekta Nagar, huko Narmada nchini India Guterres amesema wakati huu ambapo dunia inakabiliwa na changamoto lukuki ni wakati muafaka wa kuweka msisitizo katika kuitunza sayari dunia.

“Hakuna changamoto kubwa inayokabili dunia kwa sasa zaidi ya mabadiliko ya tabianchi, lakini mpango huu wa mitindo ya Maisha kwa kuzingatia mazingira umetengenezwa ili kuangaza ukweli muhimu wa kuleta matumaini ya ukweli, sisi sote tukiwa kama watu binafsi na jamii tunaweza na nilazima tuwe sehemu ya suluhisho la kulinda sayari yetu na mustakabili wetu wa pamoja.”

Mkuu huyo wa umoja wa Mataifa amesema mitindo ya maisha ya sasa inaongeza pengo kubwa la utofauti kati ya mtu na mtu huku akieleza changamoto nyingine ni utoaji wa hewa ambayo inaathiri zaidi mataifa masikini ikilinganishwa na mataifa tajiri duniani.

Na kueleza kuwa hii ndio sababu kubwa anasisitiza “Tubadili mifumo ya kiuchumi na iwe rafiki kwa sayari yetu na  kuwafanya watu wote wawe sawa, ili wote tupate fursa sawa ya kustawi.  Kila mmoja wetu atalazimika kujifunza kuishi kwa njia endelevu na kupunguza uharibifu wa mazingira.”

Mitindo ya Maisha yenye kutunza mazingira ni ipi?

Akiwa India Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliweka katika jengo la Taj Mahal, shada la maua kaitka kumbukumbu ya waathirika wa shambulio la kigaidi la tarehe 26/11  Akiwa India Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliweka sh…
UN
Akiwa India Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliweka katika jengo la Taj Mahal, shada la maua kaitka kumbukumbu ya waathirika wa shambulio la kigaidi la tarehe 26/11 Akiwa India Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliweka shada la maua katika jengo la hoteli ya Taj Mahal, kukumbuka waathirika wa shambulio la kigaidi la tarehe 26/11

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema ametaja namna ya kupunguza uharibifu wa mazingira na kuishi kwa mitindo mipya ya maisha ni pamoja na kuokoa nishati na kupunguza uchafuzi wa mazingira na utupaji taka. Kupunguza matumizi ya plastiki. Kutumia maendeleo ya teknolojia kwa kutumia nishati mbadala, safi kwa kupikia , chakula kilicholimwa kwenye kwa kuzingatia uendelevu wa mazingira na kutotupa chakula.

Amesema pia ni vyema kuweka msisitizo na kuwadai viongozi waunge mkono mitindo hii safi ya maisha pamoja na kuja na hatua kabambe za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. “Huu utakuwa ni mtindo wa maisha ambao natumai unaweza kuenea ulimwenguni kote.”

Guterres amerejelea kauli iliyotolewa na Mwanamapinduzi na mpigania haki wa India Hayati Mahatma Gandhi kwamba “Dunia inauwezo wakutosha kwa hitaji la kila mtu, lakini haitoshi kwa uchoyo wa kila mtu.”  Akihisisitiza kuwa kama jamii itaweka ubinafsi pembeni na kujali umoja na manufaa ya wote basi rasilimali zilizopo zitaweza kutumika kwa heshima na kukidhi watu wote.

India Rais wa G20

Katibu Mkuu Guterres ameipongeza India kwakuwa mstari wa mbele kuweka msisitizo kwenye matumizi ya nishati mbadala huku akitaja mradi mkubwa wa Muungano wa kimataifa wa nishati ya jua.

Nchi ya India hivi karibuni itakuwa rais wa kundi la nchi Tajiri zaidi duniani G20, na kusema kuwa kwa uwezo wa rasilimali walizonazo pamoja na ujuzi  wanaweza kumaliza vita dhidi ya asili na kuwa mfano wa kuigwa wa Maisha endelevu.

Guterres pia amegusia umuhimu wa kuacha matumizi ya mafuta ya kisukuku kwani ni hatari kwa mazingira na yanadhibitika kuwa na madhara makubwa kwa ulimwengu na kukumbusha umuhimu wa kila nchi kuhakikisha yanasitisha matumizi ifikapo muda waliojipangia.

“Ulimwengu unaitegemea India na mataifa mengine ya G20 kuongoza njia katika kukomesha uraibu wetu wa matumizi ya makaa ya mawe ifikapo mwaka 2030 katika nchi za OECD na 2040 katika nchi zisizo za OECD.” Amesema Guterres na kuongeza kuwa nchi zilizoendelea lazima zifuate ahadi zao za kutoa usaidizi wa maana wa kifedha na kiteknolojia kwa nchi kama India kupitia mabadiliko haya.

Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akitoa hotuba yake katika Taasisi ya Teknolojia ya India mjini Mumbai, India
UN /Deepak Malik
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akitoa hotuba yake katika Taasisi ya Teknolojia ya India mjini Mumbai, India

Mkutano wa COP 27

Katika kipindi cha wiki tatu zijazo mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kujadili kuhusu mabadiliko ya tabianchi COP 27 unafanyika nchini Misri ambapo wakuu wancho, wanasiasa, wanasayansi na wadau wa mazingira watakusanyika kujadili masuala mbalimbali ya mazingira.

Guterres amekumbushia umuhimu wa kuzingatia makubaliano ya Paris ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na kujenga mnepo kwa jamii zilizoathirika zaidi kwa kuwapatia fedha kama fidia ya uharibifu waliokumbana nao.

Kurekebisha. Kupunguza. Fedha. Na hasara na uharibifu. Utekelezaji kamili wa ahadi za kifedha zilizofanywa huko Paris. 12 Kuongezeka kwa kiwango cha kuunga mkono kukabiliana na hali katika nchi zinazoendelea na maendeleo makubwa na yanayoweza kupimika katika hasara na uharibifu ni hali muhimu ili kurejesha uaminifu kati ya nchi zinazoendelea na zilizoendelea.