Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP27

Mkutano wa UN wa Mabadiliko ya Tabianchi: COP27
6 Novemba - 18 Novemba 2022: Sharm el-Sheikh, Misri
...

Ikikabiliwa na ongezeko la janga la uhaba wa nishati, halikadhalika hewa chafuzi na matukio mabaya zaidi ya hali ya hewa, COP27 inasaka kurejesha tena mshikamano kati ya mataifa na kutekeleza Mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi kwa ajili ya wakazi wa dunia na sayari dunia.

Wakuu wa nchi, serikali, mawaziri, wasuluhishi pamoja na wanaharakati wa tabianchi, mameya, wawakilishi wa mashirika ya kiraia, watendaji wa kuu wa kampuni watakutana katika mji wa pwani ya Misri, Sharm el-Sheikh katika mkutano mkubwa kuhusu tabianchi.

Mkutano huo wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, UNFCCC, COP27 utasongesha yale yaliyokubaliwa kwenye CO26 na kutoa hatua zinazoendana na kutatua dharura ya tabianchi – kuanzia kupunguza hewa chafuzi, kutekeleza ahadi za kufadhili hatua kwa tabianchi katika nchi zinazoendelea.

14 NOVEMBA 2022

Hii leo katika Habari za UN mwenyeji wako akiwa Assumpta Massoi tunamulika ugonjwa wa kisukari barani Afrika, jawabu la nishati salama Malawi, vijana na wito wao huko Sharm el- sHeikh kwenye COP27 na ujumbe wa Balozi mwema wa IFAD Sabrina Dhowre Elba.

1. Wakati dunia ikiadhimisha hii leo siku ya kisukari duniani kwa lengo la kuelimisha umma kuhusu ongezeko la mzigo wa ugonjwa huo na mikakati ya kuzuia na kudhibiti tishio lake, bara la Afrika linaonekana kuwa na changamoto kubwa ya ugonjwa huo, kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO. 

Sauti
13'4"
Unsplash/Matt Palmer

Watafiti msifungie tafiti zenu, chapisheni na sambazeni- Dkt. Chang'a

Mkurugenzi wa masuala ya utafiti na matumizi ya hali ya hewa kutoka Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania TMA Dr. Ladislaus Chang'a amesema ni vyema wataalamu wa Afrika wakaongeza kasi katika kufanya tafiti na kuzichapisha katika majarida ya kimataifa ili tafiti zao ziweze kutumika katika utungaji wa será za kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Dkt. Chang’a ameyasema hayo akiwa Sharm el-Sheikh nchini Misri kunakofanyika mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27

Sauti
2'57"
Dkt. Ladislaus Chang'a, Mkurugenzi wa Utafiti katika Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania, TMA akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa wakati wa COP27 huko Sharm el-Sheikh nchini Misri.
UN News

Wataalamu wa Afrika ongezeni kasi ya kufanya tafiti za mabadiliko ya tabianchi - Dkt. Chang'a

Mkurugenzi wa masuala ya utafiti na matumizi ya hali ya hewa kutoka Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania TMA Dkt. Ladislaus Chang'a amesema ni vyema wataalamu wa Afrika wakaongeza kasi katika kufanya tafiti na kuzichapisha katika majarida ya kimataifa ili tafiti zao ziweze kutumika katika utungaji wa será za kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
2'57"