Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mashambulio na mauaji yaliyofanywa na wanamgambo karibuni katika Darfur yashtumiwa vikali na KM

KM Kofi Annan ametoa taarifa maalumu, kwa kupitia msemaji wake,iliyoshutumu vikali mashambulio ya hivi karibuni ya kundi moja la wanamgambo wa Sudan yaliyofanyika katika makazi ya eneo la Jebel Moon, Darfur ya Magharibi ambapo iliripotiwa makorja ya raia waliuawa, ikijumuisha pia watoto wadogo. Mashambulio haya yaliwalazimisha maelfu ya raia kuhajiri mastakimu kunusurisha maisha.

Wahamiaji 800 kutoka Senegal kuhama makazi na kuelekea Gambia wakikimbia mapigano

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti ya kuwa mnamo wiki mbili zilizopita wahamiaji 800 ziada kutokea jimbo la Casamance la Senegal ya kusini wameyahama makazi yao na kukimbilia vijijini katika taifa jirani la Gambia kujiepusha na mapigano yaliofumka nchini mwao kati ya vikosi vya Serekali na waasi wanaotaka kujitenga, tangu mwezi Agosti mwaka huu.