Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

KM kuhimiza suluhu ya amani kwa Darfur

KM Ban Ki-moon amemtumia Raisi Omar Hassan Al Bashir wa Sudan, kwa mara nyengine tena barua yenye kuelezea, kwa ukamilifu, utaratibu na hatua za kuchukuliwa zitakazorahisisha ile rai ya kupeleka vikosi vya mseto vya ulinzi wa amani vya UM na AU katika Darfur, majeshi ambayo idadi yao inakadiriwa kufikia askari 24,000.

Mkataba wa CITES juu ya udhibiti wa biashara ya pembe za ndovu

Ofisi Kuu ya taasisi ya Mkataba wa Kudhibiti Biashara ya Kimataifa ya Kuhifadhi Mimea Pori na Wanyama Wanaohatarishwa Kuangamizwa - mkataba ambao hujulikana kwa umaarufu kama Mkataba wa CITES - hivi karibuni ilichapisha taarifa muhimu yenye kubainisha mapendekezo karibu 40 yanayotakikana yatekelezwe na nchi wanachama ili kurekibisha kanuni za kuendesha biashara ya viumbe pori katika soko la kimataifa.

Mkataba wa CITES juu ya udhibiti wa biashara ya pembe za ndovu

Ofisi Kuu ya taasisi ya Mkataba wa Kudhibiti Biashara ya Kimataifa ya Kuhifadhi Mimea Pori na Wanyama Wanaohatarishwa Kuangamizwa - mkataba ambao hujulikana kwa umaarufu kama Mkataba wa CITES - hivi karibuni ilichapisha taarifa muhimu yenye kubainisha mapendekezo karibu 40 yanayotakikana yatekelezwe na nchi wanachama ili kurekibisha kanuni za kuendesha biashara ya viumbe pori katika soko la kimataifa.

UM unatarajia matokeo mazuri Usomali

Eric Laroche Mshauri wa UM kuhusu Misaada ya Kiutu kwa Usomali alipokutana na waandishi habari wa kimataifa hapa Makao Makuu wiki hii aliashiria ya kwamba Usomali, kwa sasa, imebahatika kushuhudia “vuguvugu la mabadiliko” yaliyowapatia umma matumaini ya kwamba Serekali mpya itajinyakulia fursa ya utawala iliyobarikiwa karibuni na kurudisha amani na utulivu katika taifa ambalo limenyimwa uongozi wa Serekali halali tangu 1991.~~

ICC imetangaza rasmi majina ya watuhumiwa wawili wa jinai ya Darfur

Luis Moreno Ocampo, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Halaiki (ICC) ametangaza wiki hii kupokea ushahidi unaowapa madaraka ya kuwashitaki aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Sudan, Ahmad Muhammad Harun pamoja na kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Janjaweed Ali Kushayb ambao walituhumiwa “kushiriki kwenye makosa ya jinai dhidi ya raia wa jimbo la Darfur”.

Hapa na pale

Louise Arbour, Kamishna Mkuu juu ya Haki za Kibinadamu alifanya mahojiano wiki hii na wawakilishi wa vyombo vya habari waliopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UM) ambapo alionya kwamba licha ya kupatikana maendeleo karibuni katika ulinzi wa haki za kibinadamu, hususan katika mwaka huu - na kutoa mfano wa kupitishwa ule mkataba wa kupinga tabia ya kutorosha watu na kuwaangamiza - hata hivyo, yeye binafsi, alisema, anaamini bado mchango mkubwa ziada unahitajika katika sehemu nyengine za maamirisho ya haki za kibinadamu ulimwenguni, hususan katika juhudi za kukomesha kile alichokiita “msiba wa baa” la unyanyasaji na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake.~

Mazungumzo ya amani kwa Darfur yafanyika Khartoum

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani kwa Sudan (UNMIS) limeripoti kuwa Alkhamisi kulifanyika mkutano wa sita wa Utaratibu wa Amani wa Sehemu Tatu, katika mji wa Khartoum, Sudan ambapo kulijumuika wawakilishi wa Vikosi vya Ulinzi wa Amani vya Umoja wa Nchi Huru za Afrika (AU), wawakilishi wa UM pamoja na wale wa Serekali ya Sudan ambao walizingatia, kipamoja, furushi la mapendekezo ya kuimarisha zaidi operesheni za amani za vikosi vya AU katika Darfur.