Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UNDP ya Maendeleo ya Binadamu kwa 2006 yawakilishwa Afrika Kusini

Ripoti ya UNDP ya Maendeleo ya Binadamu kwa 2006 yawakilishwa Afrika Kusini

Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) limewasilisha rasmi Alkhamisi mjini Cape Town, Afrika Kusini Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu kwa 2006 iliyopewa muktadha usemao “Upungufu wa mahitaji uliovuka mipaka: mzozo wa maji ulimwenguni, ufukara na nguvu za mamlaka.”

Kadhalika ripoti ya UNDP ilifafanua orodha ya mipango ya maendeleo ya binadamu inaotegemea kuwepo fungamano katika huduma za maji na usafi wa makazi. Vile vile ripoti ilikadiria viwango vya maendeleo kwa kutumia kiashirio kilichopima natija za maendeleo kwa umma, kwa ujumla, mathalan, ilitathminia namna hali ya maisha inavyoathiri umri wa mtu wa kawaida na kupima jumla ya mapato kwa kila mtu. Kiashirio cha UNDP, kwa bahati mbaya, kilithibitisha matarajio ya muda wa kuishi katika sehemu ya Afrika, kusini ya Sahara, yaliteremka katika kipindi cha hiv sasa tukilinganisha na miaka 30 iliopita kwa sababu ya kutanda kwa janga la UKIMWI katika eneo hilo.