Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wapongeza upigaji kura shwari wa uraisi katika DRC

UM wapongeza upigaji kura shwari wa uraisi katika DRC

Baraza la Usalama pamoja na KM wamewapongeza wazalendo wa JKK (DRC)kwa kufanikiwa kuendeleza upigaji kura wa duru ya pili ya uchaguzi wa uraisi nchini mwao, uliofanyika mwisho wa Oktoba, kwa utulivu wa amani.

Baraza la Usalama limeahihidi kuwa UM na mashirika yake yataendelea kutoa msaada kwa DRC katika huduma za kufufua tena taasisi zake za utawala na uchumi maendeleo.