Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM anaamini Afrika itafaidika kimaendeleo ikijifunza namna ya kupunguza ufukara kutoka kwa Wachina

KM anaamini Afrika itafaidika kimaendeleo ikijifunza namna ya kupunguza ufukara kutoka kwa Wachina

KM wa UM Kofi Annan ameipongeza Uchina kwa kuahidi kuongeza, kwa mara mbili zaidi, misaada ya maendeleo kwa bara la Afrika itakapotimia 2009. Ahadi hii ilifikiwa na wawakilishi wa Serekali ya Uchina na viongozi wa Afrika waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Baraza la Ushirikiano wa Uchina na Afrika uliofanyika majuzi mjini Beijing.

KM alikumbusha Uchina na Afrika miaka yote "wakizungumza kwa sauti moja kuhusu lengo la kuimarisha natija za uchumi na kukuza maendeleo."