Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Didier Drogba ameteuliwa kuwa balozi mfadhili wa UNDP

Didier Drogba, mchezaji mashuhuri wa mpira kutoka Cote d’Ivoire anayechezea timu ya Chelsea ya Uingereza, na kuongoza kwa kufunga magoli mengi zaidi kushinda wachezaji wengine Ulaya hivi sasa, ameteuliwa na Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) kuwa Balozi Mfadhili, atakayesaidia kwenye zile juhudi za kuhamasisha umma wa kimataifa kujumuisha mchango wao maridhawa, ili kukamilisha, kwa wakati, yale Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

Ziara ya Katibu Mkuu katika Ikulu ya Marekani

Ijumanne KM Ban Ki-Moon alizuru Ikulu ya Marekani mjini Washington DC na kufanya mkutano rasmi, wa awali, na Raisi wa Marekani George Bush. Ziara hiyo ilihusika na hishima za kidiplomasia kwa Serekali Mwenyeji wa UM, yaani Serekali ya Marekani, ziara ambayo KM mpya anawajibika kuikamilisha.~

Baraza la Usalama lapendekeza kuchukuliwe hatua za dharura katika Jamhuri ya Afrika ya Kati

Raisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Januari, Balozi Vitaly Churkin wa Shirikisho la Urusi aliwaambia waandishi habari waliopo Makao Makuu ya UM kwamba wajumbe wa mataifa 15 katika Baraza hilo walikubaliana kupendekeza kwa KM Ban Ki-moon atayarishe haraka tume ya utangulizi itakayozuru Chad na pia Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa mashauriano na serekali za mataifa haya mawili. Baadaye KM alitakiwa atayarishe ripoti ya mapema itakaousaidia UM kuandaa operesheni za ulinzi wa amani katika eneo lao.