Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Muda wa UNMIS Sudan umeongezwa hadi 9 Julai

Wajumbe wa varaza la usalama leo wameafiki kuongeza muda wa mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ulioanzishwa wakati wa miwsho wa vita vya wenyewe kwa wenyewe baina ya Kusini na Kaskazini mwa Sudan na kuanzisha mpango mpya baada ya Sudan Kusini kujitenga rasmi mwezi Julai.

Wasomali milioni 2.4 wanahitaji msaada:UM

Umoja wa Mataifa umesema kuwa takriban watu milioni 2.4 nchini Somalia wakiwa ni asilimia 32 ya watu wote nchini humo kwa sasa wanahitaji msaada wa kibinadamu lakini idadi hii huenda ikaongezeka zaidi kutoka na mzozo unaondelea kushuhudiwa nchini humo na ukame wa muda mrefu ambao umesababisha kufariki kwa mifugo wengi.

Ban ataka uchunguzi dhidi ya mauaji Syria

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon ametaka kufanyika kwa uchunguzi kutokana na ghasia zinazoendelea nchini Syria baada ya vikosi vya serikali kuongeza matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji nchini humo.