Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM kuchunguza ukiukaji wa haki Libya

Wataalamu wa UM kuchunguza ukiukaji wa haki Libya

Timu ya wataalamu watatu wa Umoja wa Mataifa imewasili mjini Tripoli Libya kuchunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu tangu kuanza kwa machafuko mwezi Februari mwaka huu.

Timu hiyo imetumwa na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuangalia ukiukaji wa haki za binadamu baada ya serikali ya Libya kuanza kuwasaka na kuwaua waandamanaji. Serikali ya Libya imearifiwa kusema kwamba itatoa ushirikiano kwa timu hiyo ambayo itachunguza madai ya ukiukaji wa haki yakiwemo yale serikali inayosema yametekelezwa na NATO na waasi.

Timu hiyo inaongozwa na profesa Cherif Bassiouni, wengine ni Asma Khader na Philippe Kirsch na inatarajiwa kuwasilisha matokeo ya uchunguzi kwa baraza la haki za binadamu mwezi juni mwaka huu.