Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawaziri wa afya wajadili magonjwa yasiyo ya kuambukiza

Mawaziri wa afya wajadili magonjwa yasiyo ya kuambukiza

Mawaziri wa afya kutoka kote duniani leo wameanza mkutano wa siku mbili mjini Moscow Urusi ili kujadili magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO mkutano huu ni muhimu sana kwa kampeni ya kimatafa kukabiliana na maradhi hayo ikiwemo saratani, maradhi ya moyo, kisukari na magonjwa sugu ya mapafu.

Mkutano huo umeandaliwa na serikali ya Urusi na WHO na lengo kubwa ni kuzisaidia nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuanzisha na kuimarisha sera na mipango kuhusu maisha yanayozingatia misingi ya afya na kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Magonjwa haya yanakatili maisha ya mamilioni ya watu kila mwaka na waathirika wakubwa ni nchi za kipato cha chini na cha wastani. Profesa P. Anyang'nyong ni waziri wa afya wa Kenya na ni miongoni mwa wanaohudhuria mkutano huo.

(SAUTI YA P. ANYANG'NYONG)